SHIRIKA LA AGAPE ACP LATOA MSAADA WA VIFAA KUKABILIANA NA CORONA VIJIJI VYA KATA YA MWAMALA SHINYANGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola (kushoto) akimkabidhi ndoo ya kunawia mikono Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Shirika limetoa msaada wa ndoo 62, sabuni 62 za maji na barakoa 150 kwa ajili ya kusaidia wananchi wa vijiji vya kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona.  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola (kushoto) akimkabidhi ndoo ya kunawia mikono Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. 
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akijaribishia kufungua ndoo ya kunawia mikono.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola (kushoto) akimkabidhi sabuni za maji kwa ajili ya kunawia mikono Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola (kushoto) akimkabidhi barakoa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola akizungumza wakati wa akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mchango wa vifaa  kwa ajili ya kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Corona.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akilishukuru Shirika la AGAPE kwa kutoa mchango wa vifaa  kwa ajili ya kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Corona huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidiana na serikali kukukabiliana na COVID -19. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akizungumza wakati akipokea msaada wa ndoo 62,sabuni 62 za maji na barakoa 150 zilizotolewa na Shirika la AGAPE ACP kwa ajili ya kusaidia wananchi wa vijiji vya kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kuiunga mkono serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona. 
Muonekano wa sehemu ya ndoo, sabuni na barakoa zilizotolewa na shirika la AGAPE ACP.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Agape ACP limetoa msaada wa ndoo 62, sabuni 62 za maji na barakoa 150 kwa ajili ya kusaidia wananchi wa vijiji vya kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kuiunga mkono serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona. 

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko leo Jumatatu Mei 11,2020, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola amesema vitaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona. 

“AGAPE ACP kwa kushirikiana na kamati za MTAKUWWA tumekuwa tukitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na madhara ya mimba na ndoa za utotoni lakini sasa pia tutatoa elimu kuhusu Corona kwani huenda katika kipindi hiki cha Corona kuna vitendo vya ukatili wanafanyiwa watoto”,alieleza Myola. 

“Kwa kuwa tunatekeleza mradi wa Utu wa Msichana kwa ufadhili wa shirika la MUNDO Co-Operante katika kata ya Mwamala tumeona ni vyema tuchangie ndoo za kunawia mikono,sabuni za maji na barakoa ambavyo tutavigawa katika vijiji vinne vya kata ya Mwamala,zahanati na familia duni zitakazotambuliwa na serikali ya kijiji kuwa hazina uwezo wa kununua vifaa vya kupambana na Corona”,aliongeza Myola. 

Akipokea mchango huo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amelishukuru Shirika la AGAPE kwa kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Corona huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidiana na serikali kukukabiliana na COVID -19. 

“Tunawashukuru AGAPE ACP kwa mchango huu na upendo wenu kwa wananchi wa Shinyanga. Mkienda Mwamala hakikisheni mnawasisitiza wananchi wanawe mikono kila wanapohitaji kupata huduma za kijamii wasishike kitu bila kunawa”,alisema Mboneko. 

“Wasisitizeni wazazi na walezi kulinda watoto wao wasizurure minadani bali watulie majumbani na wajisomee wasiwaozeshe na wananchi wasitumie barakoa zilizotengenezwa kwa mifuko ya plastiki”,aliongeza Mboneko.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464