Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Jumanne
WATU wanne wilayani Ukerewe, Mkoa wa Mwanza wamefariki huku wengine
27 wakijeruhiwa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria katika Ziwa
Victoria kupigwa na radi.
Akizungumza jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP. Muliro
Jumanne amesema, tukio hilo limetokea Juni 23 mwaka huu saa 2 na dakika
45 asubuhi katika Kitongoji cha Busele, Kata ya Bubiko, wilayani
Ukerewe mkoani Mwanza.
Muliro amesema, mtumbwi huo wa abiri unaojulikana kama One Ten wenye
namba za usajili 00238 unaofanya safari za Kond na Bugaza ulipigwa radi
na kusababisha vifo vya watu wanne pamoja na majeruhi 27 ambapo kati yao
ni wanawake 12 na wanaumme 15.
Alitaja majina ya waliofariki kuwa ni alikuwa ni Nahodha wa mtumbwi
huo Kumunya Andrea(36), Simon Charles (36) Nahodha msaidizi pamoja na
Ndege Abdu(25), Deogratus Mulungu(50).
Pia amesema, majeruhi wamefikishwa katika Zahanati ya Kijiji cha
Bukiko na wengine Kituo cha Afya cha Bwisya kwa ajili ya matibabu, huku
baadhi wametibiwa na kuruhusiwa.
Miili ya marehemu wote imefanyiwa
uchunguzi na daktari na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya taratibu za
mazishi.
CHANZO - TIMES MAJIRA
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
CHANZO - TIMES MAJIRA