Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Shinyanga Mjini, limelaani tukio la Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, kushambuliwa na watu wasiojulikana akiwa Jijini Dodoma na kuvunjwa mguu.
Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2020 na Mwenyekiti wa baraza hilo Samsoni Ng'wagi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Taifa, linapaswa kupingwa na kila mtu.
“Sisi baraza la vijana la CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini, tunalaani tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wetu wa Taifa Freeman Mbowe Juni 9 mwaka huu akiwa Jijini Dodoma na watu wasiojulikana. Tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchuguzi wa kina juu ya tukio hilo",” alisema Ng’wagi.
Kwa upande wake Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Shinyanga Alfredy Masanja, alisema CHADEMA itaendelea kupigania maslahi ya Watanzania, huku akiwataka viongozi na wanachama kuendelea kusimama imara.
Katika hatua nyingine aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kufanya kazi yao kwa weledi hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
TAZAMA PICHA
Mwenyekiti wa Baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Shinyanga mjini Samson Ngw'agi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari na kulaani tukio la Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe, kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Katibu wa BAVICHA wilaya ya Shinyanga Alfred Masanja, akizungumza na wana habari
Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA wakiwa kwenye kikao chao, na waandishi wa habari.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la vijana BAVICHA wakiwa kwenye kikao chao, na waandishi wa habari.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464