Wanasayansi
wanafanya majaribio kuona iwapo dawa ya maumivu ya Ibruprofen inaweza
kutumika katika hospitali kuwasaidia wagonjwa wa corona.
Kikosi
hicho katika hospitali ya Guys and ST Thomas and College kinaamini
kwamba dawa hiyo , ambayo hutumika kumaliza maumivu inaweza kutibu
matatizo ya kupumua.
Wanaamini kwamba dawa hiyo isio na gharama ya juu inaweza kuwasaidia wagonjwa kutowekwa katika mashine za kuwasaidia kupumua.
Katika vipimo hivyo kwa jina Liberate, nusu ya wagonjwa watapatiwa dawa ya Ibuprofen kabla ya kuafnyiwa uangalizi wa kawaida.
Majaribio hayo yatatumia ibuprofen maalum badala ya ile ya kawaida ambayo watu hununua.
Baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitumia dawa hiyo aina ya capsule kutibu magonjwa kama vile baridi yabisi.
Utafiti
uliofanyiwa wanyama unasema kwamba inaweza kutibu tatizo la kupumua
-tatizo kubwa miongono mwa wagonjwa wa corona walio katika hali
mahututi.
Profesa Mitul Mehta , mmoja wa wanachama wa kikosi hicho
katika taasisi ya Kings College mjini London alisema: Tunahitajika
kufanya majaribio ili kuthibitisha kwamba ushahidi unafanana na kile
tunachotarajia.
Mapema wakati wa mlipuko huo kulikuwa na hofu
kwamba Ibruprofen inaweza kuwa mbaya kwa matumizi ya wagonjwa iwapo
watakuwa na dalili hafifu.
Wasiwasi huo uliongezeka baada ya
waziri wa afya nchini Ufaransa Olivier Veran kusema kwamba dawa kama
Ibuprofen , zinaweza kuongeza maambukizi na akawataka wagonjwa kutumia
dawa aina ya paracetamol badala yake.
Uchunguzi uliofanywa na tume
ya dawa za binadamu ulibaini kwamba Paracetamol , ilikuwa salama
kutumia kukabiliana na dalili za corona.
Dawa zote mbili zinaweza kupunguza viwango vya joto mwilini na kukabiliana na dalili zinazohusishwa na homa ya flu.
Kwa
dalili hafifu za corona , Idara ya afya nchini Uingereza inawashauri
watu kutumia dawa aina ya paracetamol kwanza kwa kuwa ina madhara
machache badala ya Ibuprofen na ni chaguo salama kwa watu wengi.
Hufai kutumia Ibuprofen iwapo una vidonda tumboni kwa mfano.
https://www.bbc.com/swahili/habari