
Na mwandishi wetu,Shinyanga Press Club Blog
Watu nane wamepoteza maisha
katika ajali ya gari na wenginewatano kujeruhiwa
baada ya Lori mali ya Texas Hardware kugonga Tela la trekta kwa nyuma na kukosa
mwelekeo kisha kuligonga gari la abiria na kusababisha vifo.
Ajali hiyo ilitokea jana Juni 10 majira ya saa 9:45 usiku katika
barabara ya Mwanza -Musoma eneo la Ihayabuyaga Kata ya Bukandwe wilayani Magu
mkoani Mwanza ambapo tayari wanamshikilia dereva wa lori Boniphace Cliphord Tuju(37) mkazi wa mwanza-Nera
Taarifa iliyotolewa leo Juni 11 na kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa
wa Mwanza Jumanne Muliro imesema kuwa, dereva huyo alikuwa anaendesha gari
lenye namba za usajili T.322 DCB na Trailer T.1351 DCA na lilikuwa likitoka
wilaya ya Busega kwenda Mwanza.
Kamanda Muliro amesema Lori hilo liligonga tela ya trakta kwa nyuma ambayo ilikuwa haina
taa za nyuma yenye namba za usajili T.952
DGW, baada ya kuligonga ilihama njia na kugongana na gari iliyokuwa na
abiria kutoka mwanza kwenda magu yenye namba za usajili T.775 DEG.
Alisema gari ya abiria aina ya nissan inayomilikiwa na george philipo@msangi ambaye alikuwa dereva
wa gari hiyo ambaye alifariki kwenye ajali na abiria wake waliopoteza maisha
wote wakiwa ni wanaume na watano kujeruhiwa.
Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na miili
yao kutambuliwa ni George Msangi dereva wa Hiace mkazi wa Magu,Hamis Masige(35)
mwalimu wa Luhenge secondary mkazi wa Lugeye na waliofariki wengine 6 bado
hawajatambulika wote ni wanaume.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wanapatiwa
matibabu hospitali ya Bugando kuwa ni Ayubu Mindule Mratibu elimu Kata ya
Chabula mkazi wa nyanguge,Elias Lutandula(46)mkulima mkazi wa Nyanguge.
Wengine ni
Kasabuku Kishela(32)msukuma mkazi wa Magu, Edibini Makubo (20) mwanafunzi wa kidato
cha sita Bariadi high school mkazi wa Nyanguge na Elias Francis(44)mkazi wa nyanguge ambaye amelazwa
hospitali ya Magu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464