KKKT LAJITOSA VITA DHIDI YA CORONA, LAGAWA VIFAA KWA WAKUU WA MAJIMBO NA WACHUNGAJI


Na Marco Maduhu - Shinyanga Press Club Blog

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Masharika ya Ziwa Victoria, limetoa vifaa vya kisasa kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa hilo, kutoka Shinyanga na Simiyu, kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Zoezi la utoaji wa vifaa hivyo limefanyika leo Juni 23, 2020 katika kanisa la KKKT Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu hao wa majimbo pamoja na wachungaji, huku pia ikiendeshwa ibada fupi ya kuweka wakfu vifaa hivyo pamoja na kuliombea taifa kuondokana na virusi hivyo vya Corona.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Askofu Emmanuel Makala, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kuzingatia maelekezo ya Serikali, kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa, kupaka vitakasa mikono ili waendelee kuwa salama.

“Natoa wito kwa wananchi wasividharau virusi vya Corona, bali waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga pamoja na kufuata maelekezo ya Serikali, kwa kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka, kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu wengi na kutokaa makundi,” amesema Makala.

Aidha amevitaja vifaa ambavyo wamevitoa, kuwa ni Barakoa, Sabuni, pamoja na vifaa vya kisasa vya kunawa mikono kwa majitirika bila ya kugusa koki ya maji wala sabuni, bali vinatumika kwa kukanyaga kwa miguu, kwa kushirikina na kanisa la kiluther Bavaria la ujerumani ili kuendelea kuchukua tahadhari zaidi, 

Naye Mchungaji Patric Zengo wa usharika wa Kanani (KKKT) Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, akizungumza kwa niaba ya wenzake, ameshukuru msaada wa vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia kuendeleza mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa waumini wao. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Shinyanga na Simiyu, Emmanuel Makala, akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya kukabiliana na Corona.
Askofu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Shinyanga na Simiyu, Emmanuel Makala, akinawa mikono wa sabuni na majitiririka kabla ya kuanza kugawa vifaa hivyo, vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Askofu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Shinyanga na Simiyu, Emmanuel Makala, akiweka wakfu vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kabla ya kuanza kuvigawa.
Askofu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Shinyanga na Simiyu, Emmanuel Makala (kulia),akimkabidhi vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona mchungaji Patric Zengo usharika wa Kaanani Ndembezi kwa niaba ya wenzake.
Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Shinyanga na Simiyu, Emmanuel Makala (kushoto),akimkabidhi vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona mchungaji Patric Zengo usharika wa Kaanani Ndembezi. 
Askofu Emmanuel Makala akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Zoezi la ugawaji vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona likiendelea.
Zoezi la ugawaji vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona likiendelea.
Muonekano wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka ili kuendeleza mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Wachungaji na wakuu wa majimbo wakiwa wamebaba barakoa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na virusi vya Corona.
Wachungaji na wakuu wa majimbo wakiwa wamebaba barakoa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na virusi vya Corona.
Askofu Emmanuel Makala, katikati mwenye vazi jeupe, akipiga picha ya pamoja na wakuu wa majimbo na wachungaji, mara baada ya kumaliza kuwakabidhi vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Picha zote na Marco Maduhu 















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464