MBIO ZA URAIS ZANZIBAR ZAZIDI KUNOGA, HAMAD MASAUNI NAYE AJITOSA


Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akionyesha fomu aliyochukua kuomba kuteuliwa kugombea urais Zanzibar

Na Mwandishi Wetu - Shinyanga Press Club Blog

Mbio za kuwania urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar zimezidi kunoga kutokana na wanasiasa mbalimbali mashuhuri na makada wa chama hicho kuzidi kujitokeza kuchukua fomu.

Kati ya waliojitokeza leo Juni 22, 2020 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni ambaye amechukua fomu hiyo kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Zanzibar.

Baadhi ya makada wengine ambao tayari wameshachukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM ni Balozi Ali Karume, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha S. Jecha, Omar Sheha na Mwanamama Mwantumu Mossa Sultan.

Mhandisi Masauni akikabidhiwa fomu leo Juni 22, 2020
Mhandisi Masauni akiwasili makao makuu ya CCM visiwani Zanzibar kuchukua fomu
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464