Nahodha wa Simba SC, John Bocco akiifungia timu yake bao la pili jana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
BAADA ya wiki iliyopita Serikali kuizuia klabu ya JKT Tanzania kuingiza mashabiki katika uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri jijini Dodoma kufuatia kukiuka masharti ya afya wakati wa mchezo wake na Yanga, hatimaye timu ya Mbeya City nayo imekumbana na adhabu hiyo siku moja baada ya mchezo wake na Wekundu wa Msimbazi Simba uliochezwa jana Juni 24, 2020 kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Katika hatua nyingine Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imepiga marufuku michezo yote inayozihusisha timu za Simba na Yanga zitakazochezwa nje ya Dar es Salaam kuingiza mashabiki uwanjani, isipokuwa tu pale ambapo Serikali itajiridhisha kutoka kwa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa husika ya klabu mwenyeji.
Soma zaidi hapo chini taarifa ya Wizara iliyotolewa leo Juni 25, 2020 kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo), Shamimu Nyaki.