Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tanga imemkamata na
inamshikilia, Meneja wa Bandari ya Kipumbwi wilayani Pangani mkoani
humo, Stephen Elly Mbakweni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa
kutoka kwa mteja wake ili aweze kumruhusu kusafirisha mzigo kutoka
wilaya ya Handeni kwenda Zanzibar kupitia bandari ya Kipumbwi.
Kwa
Mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 26, 2020 na Mkuu wa Takukuru
Mkoa wa Tanga, Antony Gang'olo imesema kuwa uchunguzi wa taasisi hiyo
ulibaini kuwa Mbakweni aliomba na kushawishi hongo hiyo ikiwa ni baada
ya mteja wake kumpatia nyaraka zote zilizohitajika zilizotolewa na ofisi
ya bandari Pangani Mjini baada ya mtehja huyo kufanya malipo na
kutekeleza taratibu zingine zote zinazotakiwa na zilizowekwa kwa mujibu
wa sheria.
Gang'olo amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Soma zaidi taarifa ya Takukuru hapa chini
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464