MGODI WA BARRICK BULYANHULU WATOA MSAADA WA VIFAA WEZESHI KWA WATU WENYE ULEMAVU,KADI ZA MSAMAHA WA MATIBABU KWA WAZEE 450

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation umetoa msaada wa vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8. 

Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika leo Jumatano Juni 24,2020 katika kijiji cha Bunango kata ya Bugarama ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha. 

Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuwa ni Fimbo nyeupe 5 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho,magongo 5 na baiskeli 8 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu pamoja na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee. 

Alisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya jamii (Corporate social responsibility -CSR) unaotekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambapo walikubaliana na Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwamba asilimia 10 ya fedha ya CSR kwa ajili ya makundi maalumu vikiwemo vikundi vya akina mama,vijana,wazee na watu wenye ulemavu. 

“Vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee tulivyotoa vina thamani ya shilingi 8,050,000/= . Tunatoa shukrani kwa ushirikiano mzuri na viongozi wa ngazi zote katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya jamii hususani katika kuhudumia makundi maalumu.Tunaomba tuendelee kushirikiana kwa ajili ya kujenga jamii kwa maendeleo endelevu”,ameongeza Senkondo. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa walengwa, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ameupongeza na kuushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa wezeshi kwa wazee na watu wenye ulemavu katika kata za Bugarama na Bulyanhulu. 

“Mgodi wa Barrick Bulyanhulu mmekuwa sehemu ya familia ya wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala kutokana na ushirikiano ambao mmekuwa mkiutoa kwa jamii. Tunawashukuru kwa kuona umuhimu wa kuyafikia makundi maalumu ambayo kimsingi yanashiriki katika shughuli za maendeleo katika jamii”,amesema Macha. 

“Serikali itaendelea kushirikiana na mgodi wa Bulyanhulu na Taasisi mbalimbali katika kuyahudumia makundi maalumu kwani serikali inaamini kuwa binadamu wote ni sawa bila kujali huyu ana ulemavu au mzee.Tutaendelea kuhakikisha watu wote wanaishi kwa amani”,ameeleza. 

Mkuu huyo wa wilaya amesema vifaa hivyo wezeshi (baiskeli,fimbo nyeupe na magongo) vitawasaidia watu wenye ulemavu kuwapunguzia adha ambayo wamekuwa wakiipata katika utekelezaji wa shughuli zao za kijamii na kwamba kadi za msamaha wa matibabu zitawasaidia wazee hao 450 kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapohitaji huduma za matibabu. 

“Naomba mkavitunze na mvitumie vizuri hivi vifaa. Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hakikisha katika vituo vya afya,zahanati kuna madirisha kwa ajili ya wazee na kama hakuna hayo madirisha basi hakikisheni wazee wanapewa kipaumbele na kupewa dawa na kila mmoja anayefika hospitali akaona kuna mzee awape nafasi kwanza wazee”,ameongeza Macha. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire Amesema mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na halmashauri hiyo wamekuwa wakitekeleza mpango wa uwajibikaji kwa jamiiinayozunguka eneo la mgodi katika kata za Bugarama na Bulyanhulu ili kukuza na kuimarisha ustawi wa makundi mbalimbali ya kijamii yaliyopo katika maeneo hayo.

“Katika utekelezaji wa Programu hii ya CSR kwa mwaka 2019/2020 kwenye afua ya vijana,wazee na watu wenye ulemavu,uongozi wa kata husika uliweka vipaumbele kwenye bajeti kusaidia makundi ya wazee na walemavu vyenye jumla ya shilingi 20,000,000/= inayotolewa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu”,amefafanua. 

Kwa upande wao, Salome Samweli, Abbas Salum na Praygod Museveni wameushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kuwapatia watu wenye ulemavu baiskeli,fimbo nyeupe,magongo na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii. 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 
 Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation leo Jumatano Juni 24, 2020 katika kijiji cha Bunango kata ya Bugarama halmashauri ya wilaya ya Msalala. wa Pili kulia ni Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akifuatiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango,kata ya Bugarama ,Anna Peter na Afisa Maendeleo kata ya Bulyanhulu, Anna Boniface. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiushukuru Mgodi akiushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa wezeshi kwa wazee na watu wenye ulemavu katika kata za Bugarama na Bulyanhulu. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire, kushoto ni Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo.
Muonekano wa vifaa wezeshi (baiskeli maalumu,fimbo nyeupe na magongo kwa ajili ya watu wenye ulemavu katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 8 vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation 
Muonekano wa vifaa wezeshi (baiskeli maalumu,fimbo nyeupe na magongo kwa ajili ya watu wenye ulemavu katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 8 vilivyotolewa naMgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation. 
Muonekano wa vifaa wezeshi fimbo nyeupe na magongo kwa ajili ya watu wenye ulemavu katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation. 
Muonekano wa kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation. 
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akielezea kuhusu vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kaya ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyenye thamani ya shilingi milioni 8 vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango,kata ya Bugarama ,Anna Peter. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha. 
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akielezea namna Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unavyoshirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaozunguka mgodi huo.
 
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akiiomba serikali kuendeleza ushirikiano uliopo katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bulyanhulu na Bugarama wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa wezeshi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akiwakabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Mkuu huyo wa wilaya aliwasihi watu wenye ulemavu kutunza vifaa hivyo (baiskeli,magongo na fimbo nyeupe) ambavyo vitawasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akisalimiana na watu wenye ulemavu  wakati akiwakabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wa kata ya Bulyanhulu na Bugarama na halmashauri ya wilaya ya Msalala wakipiga picha ya kumbukumbu na watu wenye ulemavu baada ya kuwakabidhi vifaa wezeshi (baiskeli).
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wa kata ya Bulyanhulu na Bugarama na halmashauri ya wilaya ya Msalala wakipiga picha ya kumbukumbu na watu wenye ulemavu baada ya kuwakabidhi vifaa wezeshi (magongo na fimbo nyeupe).
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akielezea kuhusu kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee 450 wanaoishi katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akionesha sehemu ya kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee wanaoishi katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi  kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mmoja wazee hao akifurahia kadi ya msamaha wa matibabu baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiangalia kadi ya msamaha wa matibabu kabla ya kumkabidhi mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi  kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi  kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi  kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi  kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Watu wenye ulemavu wakiwa kwenye baiskeli walizopewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Wazee na Watu wenye ulemavu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
 Abbas Salum akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kutoa msaada wa baiskeli,fimbo nyeupe,magongo kwa watu wenye ulemavu na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii. 
 Mzee Praygod Museveni akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kutoa msaada wa baiskeli,fimbo nyeupe,magongo kwa watu wenye ulemavu na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii. 
Salome Samwel akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kutoa msaada wa baiskeli,fimbo nyeupe,magongo kwa watu wenye ulemavu na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii. 
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. 
Afisa Tarafa ya Msalala,Victoria Lusana akiushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwapatia vifaa wezeshi watu wenye ulemavu na wazee katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu.
Afisa Mawasiliano Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464