MKUU WA TAKUKURU ARUSHA ARUDISHWA MAKAO MAKUU, WENGINE WATANO WAHAMISHWA VITUO



Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia John Mbungo

Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) makao makuu leo Juni 27, 2020 imefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya viongozi na watumishi, ambapo miongoni mwa waliohamishwa kikazi ni aliyekuwa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi ambaye amehamishiwa makao makuu.

Nafasi yake inachukuliwa na James Ruge ambaye anatoka ofisi ya Mkurugenzi Mkuu makao makuu, ambapo Ruge anakwenda kuwa Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoani Arusha.

 Mabadiliko hayo yamefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia John Mbungo ambapo mabadiliko hayo yamewahusisha watumishi sita wa taasisi hiyo wakiwemo watano kutoka mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Juni 27, 2020 na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Doreen Kapwani imesema kwamba Frida Wikesi anahamishwa na kurudishwa makao makuu ambako atafanya kazi kitengo cha Kurugenzi ya uchunguzi.

Wengine waliobadilishiwa vituo vya kazi ni Mkuu wa Takukuru wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Deogratius Peter anayehamia wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, huku Zawadi Ngailo aliyekuwa Arumeru akipelekwa ofisi ya Takukuru mkoa wa Arusha.

Soma zaidi taarifa hiyo hapa chini




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464