- Mkuu wa wilaya ya Kahama , Anamringi Macha akiongea katika kikao cha mwisho cha Baraza la Madiwani kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama ,Anderson Msumba na kushoto ni aliyekuwa mwenyekiti wake Abel Shija , Picha na Patrick Mabula.,
- Kahama Mkuu wa wilaya ya Kahama , Anamringi Macha amewataka madiwani wanaokwenda kutetea nafasi zao baada ya Mabaraza kuvunjwa kwenda kufanya siasa za kistarabu na kuacha jazba na mihemuko ili uchaguzi uwe wa huru na haki Akiongea katika kikao cha mwisho cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama kabla ya kuvunjwa amewataka wanaokwenda kutetea nafasi zao kuacha jazba na kufaata sheria , kanuni na taratibu zilizopo kwenye vyama vyao vya siasa.Macha amesema siasa siku zote inamhemko na kuwataka kwenda kuwa watulivu na wastarabu katika kata zao kwa kufuata sheria na kanuni katika mchakato wa kugombea wasije wakaenda kinyume na taratibu za chama na kujikuta wanakosa sifa za kuteuliwa.Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama , Anderson Msumba amesema miradi yote iliyoanzishwa wataikamilisha kwa wakati na kuwatakia kila la kheri madiwani wote waweze kuchanguliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu na kuweza kurudi wote.Halmashauri ya mji wa Kahama yenye kata 20 ilikuwa jumla ya madiwani 27 kati ya hao mmoja alikuwa wa CHADEMA huku wa viti maalumu wakiwa 7 na wote ni kutoka Chama cha Mapinduzi ( CCM ).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464