MTOTO mmoja aliyetambulika kwa jina la Dalaile Milambo (6) mwanafunzi
wa chekechea, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza amefariki baada ya
kushambuliwa na fisi.
Akizungumza jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP.
Muliro Jumanne amesema tukio hilo lilitojea Juni 22, mwaka huu saa moja
jioni katika Kijiji cha Mwampuru Kata ya Mwantare wilayani Kwimba.
Muliro amesema mwanafunzi huyo wa shule ya chekechea ya Mwampuru
alifariki baada ya kushambuliwa na fisi sehemu mbalimbali za mwili wake
wakati alipokuwa na dada yake.
Amesema, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori
na wananchi wanamsaka fisi huyo ili adhibitiwe kwa mujibu wa sheria na
kuhakikisha kuwa haleti madhara zaidi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464