
Msichana Bahati Ningha aliyeomba radhi kwa kumchafua Mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime kuwa amembaka na Kumlawiti.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw Elias Ntiruhungwa aliyetuhumiwa kumbaka Mwajiriwa wake.
Msichana mwenye umri wa Miaka 19 aliyefahamika kwa majina ya Bahati Niga Mkazi
wa Shinyanga ambaye ni mtumishi wa halmashauri ya Mji wa Tarime amekanusha
taarifa zilizosambaa katika mitandao ya
Kijamii kuwa amebakwa na kulawitiwa na mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Mji
wa Tarime Bw Elias Ntiruhungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Shinyanga Msichana
huyo amesema kuwa kumekuwapo na taarifa nyingi katika mitandao ya Kijamii
zikimhusisha yeye kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri wake ambaye ni
mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime ambapo amebainisha kuwa jambo hilo
siyo la kweli ila lilifanyika kutokana
na shinikizo la baadhi ya watu kwa lengo la kumchafua mkurugenzi huyo.
Bahati amesema kuwa baada ya mtu mmoja aliyekuwa akifanya
kazi katika halmashauri hiyo (Mzee Samweli Chomete) aliyekuwa akishirikiana na
baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara kwa
utovu wa nidhamu ndipo alipoamua kumtumia yeye kwa kumlaghai kuwa ajitangaze
kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri wake kitendo ambacho kimemfadhahisha na kuidhalilisha familia
yake.
“Katika kufanikisha hili waliniondoa nilipokuwa naishi
awali na kuhamishiwa kwa mzee Chomete ili kufanikisha ushawishi wao ambapo wanizuia
hata kutoka na kufanya mawasiliano ya aiana yoyote”amesema Bahati
Bahati ameongeza kuwa aliahidiwa kiasi cha shilingi
milioni 50 toka kwa baadhi ya wanasiasa Mjini Tarime kuwa endapo atafanikiwa
kutimiza lengo la kuondolewa kwa Mkurugenzi huyo kwa kashfa ya ngono, atapewa
pesa hizo.
Katika hatua
nyingine Bahati amesema kuwa katika maisha yake yote aliyoishi Tarime hajawahi
kuwa na mahusiano ya aina yoyote ya kimapenzi na Mwajiri wake kama ilivyoenea mitandaoni.
Amesema kuwa ameamua kuuambia umma ukweli kuwa jambo hilo
lilifanyika kwa shinikizo la baadhi ya watu kwa lengo la kumchafua mkurugenzi
wa mji Tarime Bw Elias Ntiruhungwa ili aweze kuondolewa katika halmashuari hiyo
kwa njia ya kufukuzwa kazi au kuhamishwa kutokana na tuhuma za ngono na
ubakaji.
Hata hivyo Bahati ameiomba radhi Serikali na familia ya Mkurugenzi huyo wa Mji
Tarime kwa usumbufu wowote uliyojitokeza
kutokana na habari hizo ziliozenea
kwenye miandao ya Kijamii ambapo hakujua ukubwa wa athari zake.
Kwa upande wake Mama Mzazi wa Bahati Bi Amina Kassim ambaye amezungumza na vyombo vya habari ameeleza
kusikitishwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijaamii kuwa mwanae amebakwa
na kulawitiwa jambo lililowasukuma kufunga safari kuelekea Mjini Tarime
kujiridhisha na taarifa hizo ambapo alimkuta mwanae akiwa mzima wa afya huku
akisema kuwa tukio na taarifa hizo zilitolewa na watu wasio kuwa na nia njema
na maisha ya Mwanae ambapo ameitaka
jamii kutokumwelewa Mtoto wake vibaya.
Bw. Petro Leonard Masato ambaye ni jirani
wa familia ya Bw. Niga amesema kuwa baada ya kupata taarifa za Msichana huyo
kubakwa na mwajiri wake zilimshitua kutokana na kuwa karibu na familia hiyo aliwasialana
na wazazi wa motto wamrudishe nyumbani na baada ya kurejea alifika akiwa na afya
njema tofauti na ilivyoripotiwa awali kwenye mitandao ya kijamii
Jitihada za kumpata mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Tarime
Bw. Elias Ntiruhungwa zimefanyika ambapo amesema kuwa suala la tuhuma za yeye Kubaka
na Kulawiti mtumishi wake amezipata kupitia mitandao ya kijamii na
kusema kuwa yeye kama kiongozi wa umma na jamii anapaswa kuwa mfano wa kuigwa
hivyo jambo hilo limemsikitisha na kumsononesha sana hapaswi kulielezea zaidi
kwa kuwa serikali kupitia vyombo vyake vinavyohusika na uchunguzi vitachunguza
suala hilo kwa umakini na kubaini ukweli wa jambo hilo ili haki iweze kutendeka.
Alipotafutwa kwa njia ya simu Makamu mwenyekiti wa
halmashauri ya Mji Tarime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamisangura Bw
Bashir Abdallah amekiri kulisikia suala
hilo kupitia mitandao ya kijamii na kusema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza
zaidi kutokana na vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wake.
Naye katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Bw.
Hamis Mkaluka amesema kuwa taarifa hiyo waliipokea kwa masikitiko makubwa kuhusu
tuhuma za Mkurugenzi Mji Tarime Kubaka na Kulawiti kuhusishwa na tuhuma hizo
ambapo amevitaka Vyombo vya ulinzi na Usalama kufuatilia kwa kina suala hilo
ili ukweli uweze kubainika na haki iweze
kutendeka.
Mkaluka Ameongeza kuwa
Tarime ni sehemu yenye changamoto nyingi za kisiasa hivyo mambo
yanayoendelea yanampa wakati mgumu kubaini jambo hilo iwapo siasa inahusika
ndani ambapo ameviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya yake haraka
iwezekanavyo ili kubaini ukweli.
Wiki Kadhaa ziliyopita
zilienea taarifa katika mitandao ya Twitter na Jamii Forum zikimuhusisha Mtumishi wa halmashauri ya Mji Tarime Bi Bahati Ningha kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri
wake ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw Elisa Ntiruhungwa.