Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
KATIKA hali isiyotarajiwa, Mzee mwenye umri wa miaka 50 mkazi
wa Kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga mkoani humo aliyejulikana kwa
jina la Malembeka Jisinza, amejikata sehemu zake za siri (Kende) kwa kutumia
kisu.
Mwanaume huyo ambaye amefanya tukio hilo la kushangaza,
alijikata pia sehemu za tumbo lake juu ya kitovu.
Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wake na waandishi wa
habari leo Juni 23, 2020 mkoani Shinyanga, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo,
ACP Joseph Paul amesema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 22, mwaka huu saa 12:00
jioni katika Kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
ACP Paul amesema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tukio hilo
la kujaribu kujiua ambapo mtuhumiwa alitekeleza tukio la kujikata sehemu zake
zote za siri (kende) kwa kutumia kisu akiwa nyumbani kwake.
Kaimu Kamanda huyo wa Polisi amesema chanzo cha tukio hilo bado
kinachunguzwa, ambapo mtuhumiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na hali yake inatajwa kuwa siyo nzuri.