RAIS MAGUFULI ATANGAZA SHULE ZOTE ZIFUNGULIWE KUANZIA JUNI 29...SHUGHULI ZINGINE ZOTE ZIENDELEE










Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Dk. John Magufuli ametangaza rasmi kuwa Juni 29,2020 shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa kwa sababu ya janga la Corona zifunguliwe huku akitangaza kurejesha shughuli zote za kijamii na kimaendeleo ambazo nazo zilisimama.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 16, 2020 wakati akilihutubia na kulifunga Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma ambalo limemaliza muda wake rasmi leo.

Amesema hivi sasa nchini Tanzania maambukizi ya Virusi vya Corona yamepungua sana na hivyo shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa zifuguliwe rasmi Juni 29 mwaka huu.

"Juni 29,2020 shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa kwa sababu ya Corona zifunguliwe. Pia shughuli zote ambazo zilikuwa zimesimama kupisha janga hilo nazo tunaruhusu zianze kuanzia tarehe hiyo, maisha lazima yaendelee.Nawashukuru Watanzania wote kwa kushinda vita dhidi ya mapambano ya Corona,"amesema Rais Magufuli.

"Kwa hali ya Corona kuendelea vizuri na kweli imepungua sana.Juni 29,2020 mwaka huu shule zote zifunguliwe. Shule zote naziruhusu rasmi na maisha mengine lazima yaendelee,"amesema Rais Magufuli.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464