Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limeeleza kuridhishwa kwake na kazi za kihabari zinazofanywa na waandishi wa habari Mkoani Mtwara kutokana na kusaidia kupunguza uhalifu na kulifanya Jeshi hilo kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Mark Njera amesema hayo alipotembelewa na Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo ambapo ameeleza kuwa wanapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanahabari.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ameishauri UTPC kuangalia namna ya kujitegemea na kuwasaidia waandishi wa habari nchini kujitambua na kutumia uwezo wao kukabiliana na changamoto za ajira na ujira mdogo wanaopata kutoka kwa Vyombo vya habari wanavyofanyia kazi.
Kwa upande wake Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo amesema ni muhimu waandishi wa habari wakajenga mahusiano chanya na Vyombo vya dola ili kupata taarifa sahihi na kwa wakati ili kuwasaidia wananchi kujua matokeo ya kazi ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu nchini.
Akizungumza baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Nsokolo amemueleza mkuu huyo wa mkoa juu ya mkakati wa UTPC kuwasaidia waandishi wa habari nchini kupitia Press Club kitaaluma na kuboresha mazingira ya kazi yao na kufanya ili kusaidia Maendeleo ya Mkoa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Mark Njera akizungumza na Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo
Kushoto ni Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Mark Njera (katikati), Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mtwara, Bi. Martina Ngulumbi.
Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa