Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
SIKU tatu baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha, James Ruge akichukua nafasi ya Frida Wikesi aliyehamishiwa makao makuu, ameanza kutema cheche baada ya kuwatia watu tisa mbaroni wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Watumishi na wafanyabiashara.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 29, 2020, Mkuu huyo wa Takukuru Arusha, James Ruge aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Sifael Pallangyo (Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Arusha), Upendo Ndoros (katibu wa malezi wilaya ya Longido), Laraposho Laizer (Katibu wa Wazazi wilaya ya Longido) na Godwait Mungure (katibu wa wazazi kata ya Kikatiti wilaya ya Meru).
Wengine wanaoshikiliwa ni Mboiyo Mollel (Afisa Mtendaji Kijiji cha Takusi wilaya ya Meru), Mikidad Mollel (Mwenyekiti kamati ya pembejeo kijiji cha Takusi), Kanankira Mnyary (wakala wa pembejeo za kilimo), Gervas Mollel (mfanyabiashara kata ya Oltrumet) na Joseph Mollel (mfanyabiashara kata ya Oltrumet).
SOMA ZAIDI KUPITIA TAARIFA HIYO HAPA CHINI