Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa
Na Marco Maduhu - Shinyanga
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) mkoani Shinyanga, imetoa elimu ya rushwa ya ngono kwa wanavyuo mkoani hapa, kwa ajili ya kutokomeza vitendo hivyo.
Elimu hiyo imetolewa leo June 27, 2020 katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga, na kukutanisha wanachuo kutoka Veta, Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) na wenyeji wa chuo hicho cha ushirika.
Akitoa elimu hiyo Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa, amesema wametoa elimu hiyo ya rushwa ya ngono wa wanachuo, eneo ambalo wanafunzi wake hasa wa kike ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo, kutokana na hatima ya ufaulu wao kuwa mikononi mwa wahadhiri.
Amesema katika mkoa wa Shinyanga tangu wazindue dawati la Rushwa ya Ngono mwaka jana (2019), wameshapokea taarifa mbili za wanachuo kuombwa rushwa ya ngono, ambapo kesi zake bado zinaendelea, na kutoa wito kwa wanachuo wasiwe wasili bali watoe taarifa kwa wingi pale wanapo ombwa rushwa ya ngono na wahadhili wao.
“Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru inatoa elimu hii ya rushwa ya ngono nchi nzima, na sisi tukaamua hapa mkoani Shinyanga tutoe elimu hii kwa wanachuo wetu ambao ndio wahanga wakubwa, ili tuwe kitu kimoja kutokomeza vitendo hivi kwa kupewa taarifa,” anasema Mussa.
Naye Kaimu Mratibu wa mafunzo kutoka chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi, Samson Charles, amesema rushwa ya ngono kwenye vyuo ipo, isipokuwa kuna usiri mkubwa ambao unatawala, kutokana na mwanchuo kutaka apatiwe maksi za bure ili apate ufaulu mzuri sababu ya uzembe wake wa kujisomea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya wapinga rushwa chuoni hapo, Kombeho Wiliam, amewataka wanachuo wajikite kwenye masomo, na siyo kusubili kupewa alama za bure kwa kutoa rushwa ya ngono, jambo ambalo litasababisha nchi kupata viongozi wasio na maadili na wasio na uwezo wa kuchapa kazi sababu ufaulu wao unatokana na rushwa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Hussen Mussa, akiwataka wanachuo mkoani humo watoe taarifa pale wanapokuwa wakiombwa rushwa ya ngono na wahadhiri wao.
Kaimu Mratibu wa mafunzo kutoka chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga, Samson Charles akiwasilisha mada juu ya rushwa ya ngono vyuoni.
Mwenyekiti wa klabu ya wapinga rushwa chuo cha Ushirika Moshi tawi Kizumbi Shinyanga, Kombeho Wiliam, akiwahimiza wanafunzi wa kike kuwa makini na kujisimamia dhidi ya vishawishi kutoka kwa walimu wa kiume.
Wanachuo wakisikiliza elimu ya rushwa ya ngono kutoka Takukuru.
Elimu ya rushwa ya ngono ikiendelea kusikilizwa.
Wanafunzi kutoka vyuo vya VETA, Shycom na Ushirika wakifuatilia kwa umakini elimu ya rushwa ya ngono vyuoni.
Washiriki hao wakifuatilia mafunzo kutoka Takukuru ya namna ya kuripoti vitendo vya rushwa ya ngono .

Mwanachuo kutoka chuo cha Ualimu (Shycom) Rahel Ezekiel, akichangia mada wakati wa majadiliano.
Mwanachuo kutoka VETA, Chausiku Ipini akichangia mada wakati wa majadiliano.
Mwanachuo kutoka chuo cha ushirika Moshi tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga, Betina Mwashambwa akichangia mada katika mafunzo hayo.
Mkuu wa Takukuru mkoani Shinyanga, Hussen Mussa, (mwenye kaunda suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya rushwa ya ngono vyuoni.
Picha zote na Na Marco Maduhu