TAKUKURU YAKIRI KUWAHOJI WABUNGE 69 MATUMIZI YA FEDHA ZA CHADEMA




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) makao makuu imekiri kuwa imewaita wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya mahojiano ikiwa ni mwendelezo wa uchunguzi unaoendeshwa na taasisi hiyo juu ya malalamiko dhidi ya matumizi ya fedha za Chadema.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Takukuru iliyotolewa leo Juni 10, 2020 na Ofisa Uhusiano Takukuru Makao Makuu, Doreen Kapwani imesema fedha hizo ni zile ambazo zililalamikiwa na waliokuwa wabunge wa Chadema ambao walitangaza kukihama chama hicho katika malalamiko yao walidai kwamba walikuwa wakikatwa fedha katika mishahara yao kila mwezi kuanzia Juni, 2016.

SOMA ZAIDI TAARIFA YA TAKUKURU HAPA CHINI>>>







Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464