Kiungo wa Yanga, Balama Mapinduzi akidhibitiwa na nahodha wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa jana kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Na Mwandishi Wetu - Shinyanga Press Club Blog
Timu ya JKT Tanzania inayotumia uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kama dimba lake la nyumbani kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) imezuiwa kuingiza mashabiki kwenye michezo yake iliyosalia baada ya kukiuka masharti na kanuni za afya michezoni zilizoelekezwa na wizara ya afya baada ya kurejea hivi karibuni.
JKT imekumbana na adhabu hiyo kufuatia mchezo wake wa jana Juni 17, 2020 dhidi ya Yanga SC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kujaza mashabiki na kukaa bila kuzingatia maelekezo, hivyo kuhatarisha afya za mashabiki dhidi ya virusi vya Corona.
Soma zaidi taarifa iliyotolewa leo Juni 18, 2020 na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Lorietha Lawrence