SHIRIKA LA TCRS LATOA REDIO NA SABUNI ZA MAJI KWA WALEMAVU KUWAKINGA NA CORONA




Baadhi ya watoto wenye ulemavu Kijiji cha Ngofila wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wao pamoja na viongozi wa Kijiji na Shirika la TCRS ambalo limekabidhi msaada wa Redio,sabuni za maji za kunawia mikono kwa walemavu ili kuwawezesha kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya Corona kupitia vipindi vitakavyorushwa.



Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Caroline Kayombo akiangalia vifaa vilivyotolewa na Shirika la TCRS kwenye vijiji 24 wanapotekeleza mradi.



Na Mwandishi wetu Shinyanga Press Club Blog

Shirika la Tanganyika Christian Refugee Service(TCRS) limetoa msaada wa vifaa vya kuzuia maambukizi ya Corona kwa kaya zinazoishi na watu wenye ulemavu na taasisi za serikali zikiwemo zahanati za vijiji na shule za msingi katika kata saba za wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Akikabidhi msaada huo jana kiongozi wa mradi wa TCRS Kishapu Oscar Rutenge amesema vifaa hivyo vimepatikana kupitia ufadhili wa Shirika la Finnish Evangelical Lutheran Mission(FELM) linalofadhili miradi ya kijamii katika vijiji 24 vinavyohudumiwa na TCRS Kishapu.

Rutenge amesema kuwa watu wenye ulemavu wamewapatia Redio ili waweze kusikiliza vipindi vya elimu juu ya Corona vitakavyokuwa vinarushwa na Redio za kijamii ambazo wataingia nazo mkataba hatua ambayo itawawezesha kupata taarifa kwa urahisi.

Amesema mbali na kugawa Redio 384 kwa kaya zenye watu wenye ulemavu na Redio 30 kwa taasisi za serikali,pia Shirika hilo limetoa sabuni lita 1040 za maji kwa ajili ya kunawia mikono ambazo zitagawiwa kwa walengwa waliokusudiwa,katika vijiji 24 kutoka kata saba za Halmashauri ya Kishapu wanapotekeleza mradi.

“Pia Tumegawa sabuni ya maji yakunawia mikono lita 380 kwenye zahanati,vitakasa mikono (Sanitizer)lita tano,vitakasa mikono vya ukutani boksi nne,karatasi za kufuta maji pakti 160,ndoo za kunawisha mikono 20,barakoa N-95 na mabango ya ukutani 15 vifaa hivyo ni kwa ajili ya zahanati mbali na vilivyotolewa kwa walemavu.

Amesema pia wametoa vipeperushi 534 kwa ajili ya jamii nzima na chupa tupu 514 za ujazo wa nusu lita ambazo zitatumiwa na walengwa wa mradi watakaopatiwa sabuni kuweka kwenye chupa hizo kwa ajili ya kunawa mikono.

Alisema vifaa vyote vilivyotolewa kwa kata saba ikiwemo kata ya Shaghihilu,Ndoleleji,Masanga,Mwaweja,Mwamashele,Ngofila na Kiloleli vinathamani ya Shilingi milioni 15,317,224.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Caroline Kayombo amelishukuru Shirika hilo kwa kutoa msaada huo kwa watu wenye mahitaji maalumu,ambao utawawezesha kupata taarifa kwa urahisi za Corona na matukio mbalimbali. 


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ngofila wakiwemo watu wenye mahitaji maalumu wakisubiri kupatiwa msaada wa Redio na sabuni za maji na Shirika la TCRS la mjini Shinyanga kwa ajili ya kusikiliza vipindi vya elimu ya kujikinga na Corona. 



Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwaweja wilaya ya Kishapu Edward Ngoyeji akimkabidhi Redio mlemavu wa viungo Hellena Mahona msaada ambao umetolewa na Shirika la TCRS. 




Kiongozi wa mradi wa Shirika la TCRS Oscar Rutenge akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo kwa watu wenye mahitaji maalumu pamoja na taasisi za serikali katika kata saba za wilaya ya Kishapu,wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephat Shani na anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Caroline Kayombo. 



Wakazi wa Kijiji cha Mwaweja wakiwa wamebeba Redio walizokabidhiwa na Shirika la TCRS. 




Wakwanza ni Kiongozi wa mradi TCRS Oscar Rutenge aliyevaa tsheti ya blue,katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Caroline Kayomba na anayefuata ni Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephat Shani. 



Zoezi la kugawa vifaa likiendelea 



Watoto wenye ulemavu wakiwa na Mwenyekiti wao wa Kijiji cha Ngofila Mary Sumbula baada ya kupokea msaada wa Redio na sabuni za maji. 


Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kalitu kata ya Ngofila wakiwa wameshikilia vifaa walivyokabidhiwa na Shirika la TCRS. 


Wananchi wa Kijiji cha Mwamanota Kata ya Ngofila wilaya ya Kishapu wakiwa na vifaa walivyokabidhiwa 


Wakinamama wakiwa na watoto wao wenye ulemavu wakisubiri kupokea msaada wa Redio na sabuni za maji,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na Corona. 


Zoezi linaendelea 


Zoezi linaendelea 

Genes Tarimo kutoka Shirika la TCRS akiwaonesha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwamashele jinsi ya kutumia Radio zilizotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kupata taarifa mbalimbali kuhusu Corona. 


Zoezi linaendelea





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464