Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) kimefungua milango kwa wanachama
wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu kujitokeza kuanzia leo Juni 3 hadi Juni 15 mwaka huu.
Akiongea
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama
hicho, John Mnyika, amesema taarifa za kusudio la kugombea urais kupitia
chama hicho zinapaswa kuwasilishwa katika ofisi ya Katibu Mkuu na
baadae zitajadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kutolewa uamuzi.
“Kwa
mamlaka niliyopewa na kanuni hii ya chama ninaomba kutangaza sasa
tarehe za mwanzo wa zoezi hili na tarehe za mwisho wa zoezi hili la
kutangaza nia ya kusudio la kugombea milango hii imefunguliwa kuanzia
tarehe ya leo mpaka tarehe 15 ya mwezi Juni” amesema Mnyika
Licha
ya suala hilo la urais Katibu Mkuu huyo pia amesema kuwa chama hicho
kimefungua milango ya ushirikiano na vyama vingine kuelekea uchaguzi
mkuu wa Oktoba mwaka huu na vyama ambavyo ameviita ni vyama makini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464