Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Sigisbert Rwezaula akiwa na timu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ngazi ya halmashauri.
Na Katherine Ngowi - Kishapu
Zoezi la uwekaji wazi daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limeanza rasmi jana Juni 17, 2020, ambapo zoezi hilo litafika mwisho Juni 20, mwaka huu.

Ambapo wananchi watafika kuhakiki taarifa zao kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni katika eneo la Mhunze Stooni.
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula amesema zoezi hilo ni kwa ajili ya marekebisho ya taarifa za wapiga kura katika vituo vyote vilivyotumika katika zoezi la awali hivyo wananchi wanatakiwa kwenda katika vituo hivyo kuhakiki taarifa zao mapema.
amesema katika zoezi hilo, taarifa ambazo zitahakikiwa ni majina, jinsia, tarehe na hakutakuwa na uhamisho wa taarifa za mpiga kura kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.
Aidha, Rwezaula ametoa rai kwa wananchi wote kufika kwenye vituo walivyojiandikishia kuhakiki taarifa zao na iwapo kutakuwa na marekebisho yoyote wasisite kufika katika kituo cha Mhunze Stooni kwa ajili ya kufanya marekeshisho ya taarifa zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464