42 WAJITOSA VITI MAALUMU CCM SHINYANGA NANI NI NANI KUJULIKANA LEO



Wagombea wa Nafasi ya Viti Maalumu UWT Mkoa wa Shinyanga wakiwa wameketi kwa pamoja wakionesha Namba zao kwa wapiga kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura za maoni ili waweze kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Jumla ya Wagombea 42 wa  Nafasi ya Ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga wamejitokeza katika mnyukano wa Kusaka nafasi hiyo ambapo hii leo mapema wamejitokeza katika ukumbi wa CCM Mkoa huo kunadi sera zao kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT CCM.
Akizungumza Mapema Kabla ya kuanza kwa zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack amewahakikishia wajumbe kuwa zoezi hilo litakuwa huru na haki  ambapo kila mmoja mmoja atapata nafasi ya kunadi sera zake kwa wajumbe.
"Zoezi la Kupiga kura za maoni litakuwa ni zoezi huru  ambapo niwaombe tutumie nafasi hii kuchagua viongozi watakaotuwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na  Kutetea Maslahi ya Wanawake na watoto"
 Uchaguzi huo umeuhudhuriwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu UWT Mkoa, Wakuu wa Wilaya za Shinyanga Bi Jasinta Mboneko, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bi Nyabaganga Talaba, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya za Shinyanga Mjini na Vijijini na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi Zainab Telack

 Wajumbe wakiendelea kufuatilia sera za Wagombea ili kunakishi kile kinachoelezwa na wagombea iwapo kinawafaa na kuwaletea mabadiliko
@ShinyangaPressClub Jukwaa la Habari Tanzania 
 Uhakika wa Taarifa.
#Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440 Email : shinyapress@gmail.com

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464