Baadhi
ya miradi inayotekelezwa na shirika la IOP Mkoani Iringa ikiwemo ukarabati wa madarasa
mawili katika shule za msingi Kisoliwaya na Ilula na ujenzi wa madarasa kwa lengo
la kupunguza msongamano katika shule ya msingi Ilula.
Na Mwandishi Wetu-Iringa
Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imeyataka mashirika hayo kuwasilisha taarifa za kila robo mwaka zinazoonesha fedha na kazi
wanazozifanya kwa Msajili ili aweze kujua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yalipo mashirika hayo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Msaidizi wa Ofisi ya msajili wa NGOs, Grace Mbwilo wakati wa ufuatiliaji wa miradi
inayotekelezwa na Mashirikia Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) mkoani Iringa.
Grace amesema kuwa Serikali
inafarijika kuona mashirika yanashirikiana
nao kufanya kazi za kusaidia jamii na kutekelza miradi mbalimbali katika maeneo
waliopo kwa kufuata taratibu na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali katika eneo
husika.
Ameongeza kuwa mashirika
yanapopata fedha nyingi kutoka kwa wafadhili ili kutekeleza miradi mbalimbali
ila wanatakiwa kuhakikisha wananchi
waliokusudiwa wananufaika na miradi hiyo.
“Mwongozo tuliouzindua
hivi karibuni unasisitiza uwazi na uwajibikaji kwasababu tunajua fedha mnaomba kwa
ajili ya watanzania hivyo ni wajibu wa Serikali na Jamii husika kufahamu
zinafanya nini za zimeleta matokeo gani” alisisitiza
Aidha Mkurugenzi huyo
Msaidizi amebainisha kuwa kwa sasa NGOs
na Serikali zinashirikiana hivyo ameyasihi mashirika kutotumia njia za mkato kwani
watachelewa kufanya kazi zao hivyo kukwamisha kutekeleza miradi iliyokusudiwa
kwa wakati.
Naye Afisa Maendeleo ya
Jamii kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs, Jaina Said amesisitiza Mashirika kufuata sheria
na taratibu zilizopo kwa kutochelewesha taarifa muhimu zinazohitajika
kuwasilisha na mashirika hayo katika Ofisi ya Msajili na kusubiri faini.
“Wengine wanaona faini
ni hela ndogo, tunakupiga faini kukumbusha wajibu wako, lakini ikiwa ni zaidi ya
mara moja tunakuangalia vizuri kama unafaa” alisema Jaina.
Hata hivyo timu hiyo imelipongeza
shirika la Ilula Orphanage Program
(IOP) kwa miradi yenye lengo la kusaidia jamii hasa katika kusomesha watoto wanaoishi
katika mazingira magumu pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Akilezea utekelezaji
wa Miradi ya Shirika Ilula Orphanage
Program (IOP) Katibu Mtendaji wa Shirika hilo, Edson Msigwa
amesema kuwa Shirika lake linafanya shughuli mbalimbali za kusaidia
jamii ikiwemo kulea na kusomesha watoto,
kujenga madarasa na kuwezesha wananchi kiuchumi.
“Shirika letu lina miradi
zaidi ya 20 na kubwa tunajishughulisha na kusomesha watoto ambao ni yatima na wanaoishi
katika mazingira magumu na tayari watoto 2000 wamenufaika na mradi huo”
alifafanua.
Nayye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Ilula,Joyce Michael
amelishukuru Shirika Ilula Orphanage Program (IOP) kwa kukarabati madarasa
mawili Shuleni hapo hivyo kupunguza msongamano wa wanafunzi ambao ungeweza
kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu.
Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali akizungumza na
uongozi wa Shirika la
Ilula Orphanage Program
(IOP) kabla ya kukagua miradi inayotekelezwa na Shirika hilo,
wakati wa ukaguzi wa miradi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Iringa.
Muonekano
wa shule ya msingi Sunflower inayomilikiwa na
Shirika la Ilula Orphanage Program
(IOP) inayotumika kusomesha
watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na tayari watoto
2000 wamenufaika na mradi huo.
Picha na Kitengo
cha Mawasiliano
Serikalini WAMJW