Katibu wa CCM wilaya ya Mbogwe Bi Grace Shindika akionyesha mojawapo ya kura zilizopigwa kabla ya kuanza kuhesabiwa.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mbogwe Mkoani Geita
Augustino Manyanda Masele ameshindwa kutetea nafasi yake katika kura za Maoni
ambapo Bw Nicodemas Maganga amemshinda kwa kupata Kura 265 dhidi ya 212
alizopata Masele huku mshindi wa tatu akipata kura 16.
Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi huo Msimamzi wa
Uchaguzi Jimbo la Mbogwe ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha
mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Bw David Azalia amesema kuwa zoezi hilo limekuwa
huru na haki ambapo kila mpiga kura ameshuhudia zoezi hilo wakati kura
zikihesabiwa na kumtangaza Bw Nicodemas Maganga kuwa Mshindi wa Kura
hizo.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la
kupiga kura Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbogwe Grace Shindika
amewaambia wajumbe kuwa kura hizo si kielelezo cha ushindi kwa Mgombea bali ni
hatua ya awali ya kumpata Mgombea atakeyepeperusha Bendera ya chama hicho,
ambapo amesema kuwa mara baada ya hapo majina yatawasilishwa kwenye kamati ya
siasa ya Mkoa kisha kamati Kuu ya taifa.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe Bw
Christopher bahari aliwataka wagombea kuchagua viongozi watakaoenenda na kasi
ya Rais wa awamu ya Tano Dr John Magufuli sambamba na kuchagua kiongozi
atakayebadili na kuletamabadiliko kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutatua kero za
wananchi
Bahari
amesema kuwa nchi kwa sasa imeingia katika uchumi wa kati wa kati hivyo wanatakiwa
viongozi watakaohakikisha wanapiginia maslahi ya Umma ikiwemo kusimamia miradi
ya maendeleo pamoja na fedha zinazotolewa na serikali.
“niwaombe
katika uchaguzi huu tuhakikishe tunachagua viongozi amabao watalaeta tija na
masalahi ya umma,taifa na jamii kwani mkileta viongozi ambao ninyi mmewapanga
kwa kitu kidogo haitakusaidieni
tuleteeni viongozi watakaoinua uchumi na kutatua kero za zenu”
Aidha baada ya kutangazwa kwa kura za maoni Masele ameshindwa na Bw
Nicodemas kwa Kura 265 kwa 212 ambapo akizungumzia matokeo hayo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo
Augustino Masele amesema kuwa amepokea kwa furaha matokeo hayo na kusema kuwa
ataendelea kushirikiana na Mgombea aliyepita
Masele
amesema kutokana na demokrasia ndania ya chama hicho umesaidia zoezi kuwa huru
na kupelekea ushindi kupatikana kwa mpinzani wake wa karibu
Naye Mgombea
aliyepita katika kura hizo Nicodemas Maganga amewashukuru wajumbe wote wa Mkutano mkuu wa wilaya kwa kumuamini na kumpitisha kwa kura nyingi
ambapo amehaidi kushirikiana na Wananchi wote wa wialya hiyo katika kuleta
maendeleo ya jamii na umma
Maganga ameongeza
kuwa mara baada ya jina lake kurudi kutoka kamati kuu ya Chama taifa
atahakikisha anashirikiana na wananchi
wote wa jimbo hilo pamoja na kuondoa changamoto zinazoikabili jamii hiyo
ikiwemo migogoro ya ardhi, changamoto ya
Maji, na huduma za afya.
Jumla ya
Wagombea 31 walijitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ambapo jumla ya
Wagombea 29 walijitokeza huku wawili
wakitokomea kusikojulikana kati yao mwanamke akiwa mmoja tu huku jumla ya
wajumbe waliotakiwa kupiga wakiwa mia zaidi ya 600 ambapo waliopiga kura
walikuwa 584 moja ikiharibika Nicodemas Maganga akiongoza kwa kura 265 nafasi ya Pili ikiongozwa na Augustino Masele
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbogwe ambaye ni Katibu wa Itikadi na uenezi Mkoa wa Geita David Azalia akitoa maelekezo kwa Wajumbe na wagombea wa Mkutano mkuu wa Jimbo hilo.
Katibu tawala wa Wilaya ya Mbogwe Bw Christopher Bahari akisisitiza juu ya upatikanaji wa viongozi bora na si Bora kiongozi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Augustino Manyanda Masele Akinadi na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM katika Jimbo hilo.
Mshindi wa Kura za Maoni za mgombea wa Nafasi ya Ubunge jimbo la Mbogwe Bw Nicodemas Maganga mapema akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu.
Uhakiki wa Karatasi za kupigia kura kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza
Wagombea wa nafasi ya Ubunge jimbo la Mbogwe wakiomba Mungu Kabla ya kuanza kwa Mchakato wa Kupiga kura.
Wajumbe wakiendelea kufuatilia kujinadi kwa wagombea.
Mmoja wa Wagombea wanawake pekee ambaye amejitokeza kati ya wagombea 31 ambapo ameonyesha ujasiri kuwakabili wanaume 30.
Tazama picha mbalimbali chini
@ShinyangaPressClub Jukwaa la
Habari Tanzania
Uhakika wa Taarifa.
#Kama Una
Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 789 632 732,
+255 756 546 015 au +255 686 057 440 Email : shinyapress@gmail.com