Jumanne Sagini
Watoto wa Rais wa kwanza wa Tanzania na Muasisi wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro na Madaraka, wamejikuta kwenye mshangao baada ya kubwagwa kwenye mchakato wa kura za maoni kupata mteuliwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atakayekiwakilisha kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu katika nafasi ya ubunge wa Jimbo la Butiama mkoani Mara.
Makongoro na Madaraka walishindwa kwenye kura hizo baada ya kupata kura chache mbele ya mshindi, Jumanne Sagini ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu (RAS), ambapo ndugu hao wawili wameshindwa hata kuingia tano bora.
Makongoro Nyerere
Jimbo hilo lilikuwa na wagombea 59 na wajumbe waliopiga kura
walikuwa 555,ambapo Jumanne Sagini alipata kura 84,
akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80, wa tatu akiwa Joseph
Nyamboha kura 46.
Katika kura hizo za maoni Makongoro Nyerere alipata kura 5 na Madaraka
Nyerere aliambulia kura 2. Makongoro Nyerere aliwahi kuwa Mbunge wa
Arusha kupitia NCCR Mageuzi.
Madaraka Nyerere
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464