Naibu
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Pangani chini na ugawaji wa vitendea kazi
kwa Jumuiya hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Maji Mto Pangani,
Dkt. Victor Runyoro na kulia ni Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto
Pangani, Segule Segule.
Na Mwandishi Wetu - Pangani
NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amezindua Jumuiya ya watumiaji wa Maji Mto Pangani chini wilayani Pangani huku akizitaka vifaa vilivyokabidhiwa kwa ajili ya kufuatilia rasilimali za maji wasivitumie kama bodaboda na kupakiza nazi badala yake vitumike kwenye matumizi yaliyokusudiwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mto Pangani chini katika halfa iliyofanyika mjini humo na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro na Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Sugule.
Amesema kwamba kumekuwa na tabia jumuiya zinapokabidhiwa vifaa kwa kufuatilia rasilimali za maji huacha kufanya hivyo huku wakivitumia kwenye matumizi ambayo hayajakusudiwa huku akitoa onyo kwao.
“Ndugu zangu mmekabidhiwa vifaa hivi ikiwemo pikipiki hivyo niwatake isije kutokea bodaboda zikaenda kupakizwa nazi na popoo na kuacha kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo mtakuwa hamtendi haki na tutakaowabaini tutawachukulia hatua," alisema.
Hata hivyo amesema kwamba anaamini vifaa hivyo ambayo vimetolewa vitakuwa chachu kubwa katika jumuiya hizo kuhakikisha zinaweza kushughulikia changamoto mbalimbali.
Aidha amesema kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni lazima wahakikishe wanatimiza majukumu yao na waledi mkubwa ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza majukumu yao.
“Ndugu zangu wajibu wenu ni kuhakikisha mnasimamia ipasavyo rasilimali za maji kutokana na uwepo wa vitendea kazi hivyo mimi ni kijana wenu ikitokea mnafanya vibaya tutaivunja na kutafuta watu wengine ambao wataweza kufanya kazi kwa mujibu wa katiba iliyoasisiwa,” alisema.
Hata hivyo amewaambia kwamba yeye ni kiongozi kutoka wilayani humo hivyo lazima wahakikishe wanakuwa jumuiya ya mfano hapa nchini kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Aweso, Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Dkt Victor Runyoro amesema bonde la Pangani linasimamia wilaya 20 ambazo ni nyingi lakini kwa majukumu waliopewa kisheria na kubwa ni kuhifadhi rasiliamali maji.
Amesema kwamba maeneo mengi wanamatatizo ya maji wanapata shida sana na jinsi idadi ya watu inavyozidi kuongezaka maji kwa mtu mmoja yanadizi kupungua.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la maji la Mto Pangani Segule Segule amesema suala la utunzaji wa maji ni jukumu lao kila mmoja kuhakikisha rasilimali za maji vinatunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo
Amesema uundwaji wa jumuiya hizo zinaundwa kwa kuzingatia sheria za rasiliamali za maji ya namba 11 ya mwaka 2009 katika maelekezo ya sheria kuunganisha maelezo ya sera ya maji 2002 ambayo inataka ushirikishwaji jamii kwenye miradi na masula yote yanayohusu maji.
Mkurugenzi
wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule akizungumza wakati wa
uzinduzi huo kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Mto Pangani
Dkt Victor Runyoro kushoto ni Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya
Pangani, Seif Ally
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za
Watumia Maji Mto Pangani chini uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni
wilayani Pagani
Mwenyekiti
wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro akizungumza
wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na
kulia ni Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akijaribu moja ya vitendea kazi
vilivyotolewa kwa Jumuiya ya watumia maji Mto Pangani chini wakati
alipoizindua
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya vifaa walivyokabidhiwa