AZMINA AMIR MSHINDI KURA ZA MAONI UBUNGE VITI MAALUM UVCCM SHINYANGA

 Mshindi wa kura hizo, Azmina Amir

Na Suzy Luhende - Shinyanga
AZMINA Amir ameibuka mshindi wa kwanza katika uchaguzi kura za maoni kusaka wabunge wa viti maalum kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga katika zoezi lililofanyika leo Julai 30, 2020 ukumbi wa chama hicho mjini Shinyanga.
Azmina alichaguliwa kwa kura 13 kati ya 28 zilizopigwa na wajumbe waliohudhuria uchaguzi huo na kuwa kinara kati ya wagombea 14 waliokuwa wanawania nafasi hiyo.
Naye wa Janeth Dutu ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura sita na Leah Mbeke akiambulia nafasi ya tatu kwa kura tano.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Philemon Sengati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewataka vijana hao kuwa na ushirikiano katika uchaguzi mkuu na katika kupambana na kuleta maendeleo kwa nchi.

"Kama hatutakuwa na mapingamizi huyu mshindi wa kwanza ndiye tutakayempeleka ngazi ya juu kwenda kupambana na wenzake wa mikoa mingine," amesema Sengate.

Naye wa Janeth Dutu ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura sita na Leah Mbeke akiambulia nafasi ya tatu kwa kura tano.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Philemon Sengati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewataka vijana hao kuwa na ushirikiano katika uchaguzi mkuu na katika kupambana na kuleta maendeleo kwa nchi.
Wagombea ubunge kupitia UVCCM mkoa wa Shinyanga wakisubiri matokeo ya kura za maoni baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi UVCCM mkoa wa Shinyanga baada ya kuchagua mbunge atakayeenda kushindana ngazi ya Taifa.

Msimamizi wa uchaguzi wa ubunge UVCCM mkoa wa Shinyanga Philemon Sengate (aliyesimama) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora akitangaza matokeo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464