Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akikabidhiwa zawadi ya miwani kutoka Banda la Women in Health Sector alipotembelea banda lao katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar Es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
amewataka Wanawake wajasiriamali nchini kuchangamkia fursa na kuanzisha
viwanda vidogo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutekeleza
Uchumi wa Viwanda.
Katibu
Mkuu Jingu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea mabanda ya
wanawake wajasiriamali katika Maonesho ya 44 ya kimataifa ya Biashara
maarufu kama SabaSaba.
Amesema
kuwa hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanawake wafanyabiashara wadogo
kuanzisha viwanda ikiwa njia mojawapo ya kujikwamua kiuchumi.
Dkt.
Jingu amesema falsafa ya Rais Dkt. John Magufuli imetekelezeka kwa
vitendo na kusababisha mageuzi makubwa yaliyoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2020 badala ya lengo lililowekwa la mwaka 2025.
"Niseme
tu, wanawake wamekuwa na mchango mkubwa kuchochea maendeleo hadi hapa
tulipofika. Kundi hili ni muhimu sana katika kuendeleza na kukuza uchumi
wa taifa" alisema
Dkt.
Jingu amefafanua kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2019 Serikali
kupitia utaratibu wa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili
ya makundi maalum, imewezesha utoaji wa mikopo yenye thamani ya
Sh Bilioni 39.7 kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 870,000.
Ameongeza
kuwa katika kuhakikisha Serikali inawawezesha wanawake, katika
kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020 zaidi ya Sh Bilioni 5.6
zimewanufaisha wanawake wajasiriamali zaidi ya 17,000 kupitia dirisha
maalum la Benki ya Posta Tanzania (TPB)
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Biashara la Wanawake
Tanzania (Tanzania Women Chamber’s of Commerce), Jacquiline Maleko
amesema Serikali kwa kushirikiana na TWCC imewafikia wanawake wengi
kuwaunganisha na masoko ya bidhaa zao pamoja na kuwawezesha kupata
vibali mbalimbali
"Humu
tunao wafanyabiashara wazuri sana wenye viwango na hata wanauza bidhaa
zao katika nchi za Ulaya na Marekani ni hatua kubwa sana” alifafanua.
Mmoja
wa wajasiriamali kutoka kikundi cha, Matawi Jiko, Fausta Ntara
ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha wajasiriamali hasa wanawake kupata
mitaji na masoko ambavyo vimewasaidia kujikwamua kiuchumi.
"Tunafuraha sana kwakuwa tumekuwa katika moja ya watu muhimu katika kulifikisha taifa letu katika uchumi wa kati" alisema
TAZAMA PICHA ZAIDI
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John
Jingu akiangalia mkaa mbadala kutoka kwa kikundi cha wajasirimali
katika banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) alipotembelea
Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Dkt. John Jingu akiangalia bidhaa za wajasirimali katika Banda la Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO).
Wajasiriamali wa kikundi cha cha Jiko Matawi wakimkabidhi zawadi ya Jiko Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu alipotembelea banda la Baraza la Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) katika ya Sabasaba leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John
Jingu akiangalia huduma zinazotolewa na mmoja wa mjasiriamali katika
Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar Es Salaam.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW