DK. TULIA ACKSON ACHANGIWA SH MILIONI 3 KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE MBEYA MJINI


  Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.
NAIBU Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amesema kuwa anatarajia kuchukua fomu kesho ya kugombea ubunge Jimbo la Mbeya Mjini huku akieleza kushawishiwa na wafanyabiashara,wananchi na kuchangiwa Sh milion 3 kwa ajili ya kuchukulia fomu.

Dkt.Tulia amesema hayo jana wakati akizungumza na wafanyabishara katika soko la SIDO Jijini hapa wakati alipokuwa akikabidhiwa Sh.milioni moja ikiwa ni miongoni mwa michango aliyopatiwa na wananchi kwa ajili ya kumtuma kuchukua fomu ya kuwania jimbo hilo.

“Kutokana na kuombwa na wana-Mbeya na wafanyabishara nimeona nia yao ya dhani kwa kunichangia hivyo nimeingia katika kinyang’anyiro hicho na kesho Julai 14 nachukua fomu rasmi ya kugombea ili nikidhi kiu yao”amesema.

Aidha Dkt.Tulia alishukuru wafanyabiashara na wananchi kwa upendo waliouonyesha kwake na kuwaahidi kesho atakwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge bila kusita.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanyafabiashara Soko la Sido ,Abel Mwakipesile amesema kuwa wameamua kumchangia kiasi hicho cha fedha kutokana na jitihada zake za kujitoa kwenye jamii pamoja na kusaidia miradi ya maendeleo Jijini Mbeya.

“Sisi wafanyabiashara tumeona umuhimu wa kumchangia kuchukua fomu Dkt. Tulia kwani amekuwa akisaidia vitu mbali mbali katika jamii tena bila ubaguzi”amesema .

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Mwanamke shujaa, Sarah Ndambo amesema kuwa wao kama wanawake wanamuamini kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kupitia taasisi yake isiyo ya kiserikali ya Tulia trust inayojihusisha na uwezeshaji wa mikopo yenye riba nafuu.

Hata hivyo wanawake hao wamesema kuwa wanaimani na Dkt.Tulia kutokana na maendeleo aliyoyafanya katika kata ya majengo kwa kuwasaidia wazee wasio jiweza na kuboresha miundo mbinu ya elimu,afya na nyanja mbalimbali.

Pazia la watia nia kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi zinafunguliwa rasmi Julai kumi 14 mwaka huu huku wagombea wa chadema wakiingia katika mchakati wa kura za maoni ili kutangaza wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbio sita huku jimbo la Mbeya Joseph Mbilinyi akitetea kiti chake.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464