David Kafulila
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila na baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kisha kutumbuliwa baada ya kutia nia ya kugombea ubunge, ameshindwa kwenye kura za maoni jimboni Kigoma Kusini.
Kafulila ameshindwa kwenye kura hizo, baada ya mtia nia mwenzake, Hasna Mwilima kuibuka kidedea kwa kupata kura 273, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Nashon Bidyanguze
aliyepata kura 143 na David Kafulila akiambulia kura 64.
Kutokana na matokeo hayo, Hasna Mwilima anaweza kupata dhamana ya kuliwakilisha Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020
Kutokana na matokeo hayo, Hasna Mwilima anaweza kupata dhamana ya kuliwakilisha Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020
Katika Jimbo la Arumeru Mashariki nako aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari kisha kuvuliwa ubunge na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameangukia chali baada ya kushindwa kufurukuta kwenye kura za maoni.
Ambapo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk. John Pallangyo ameibuka kidedea katika mchakato huo kwa kura 536, huku Nassari akiambulia kura 26 pekee.
Joshua Nassari