KIKWETE: MKAPA ALINITEUA WAZIRI MAMBO YA NJE BILA HIYANA NA AMENISAIDIA SANA NIKIWA RAIS


  
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete
“Nilipokuwa Rais Mzee Mkapa amenisaidia sana, kuna wakati nikiwa Rais nilipitia changamoto kadhaa, muda mwingine mambo yalikuwa magumu kweli lakini Mzee Mkapa alisimama na mimi," Rais Mstaafu Kikwete.

“Mzee Mwinyi amepokea Tanzania uchumi wa Nchi ukiwa katika mazingira magumu amefanya jitihada kuuinua, Mzee Mkapa akaipokea Nchi uchumi ukiwa bado, akapigana sana na kipindi chake cha miaka 5 ya mwisho uchumi wa Tanzania ukawa unakuwa kwa 7%," - Mstaafu Kikwete

  “Wilaya hii ya Masasi ilikuwa na tatizo la njaa wakati ule, nikiwa Katibu CCM Masasi na DC tukabuni mradi wa kilimo cha muhogo hakikupendeza sana kwasababu Wamakuwa hawapendi sana kula ugali wa mihogo kama Mashemeji zangu Wamakonde, ila Mzee Mkapa alisimama nasi,”-MSTAAFU KIKWETE

“Wakati tunaanza mchakato wa Urais mwaka 1995 nilimueleza kuwa wewe ndiye unafaa kuwa Rais, ila baadaye nikasukumwa naamimi kugombea akanishinda, ila aliposhinda ingawa kura zetu zilikaribiana akaniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, bila hiyana,” -MSTAAFU KIKWETE 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464