James Lembeli
Na Ali Lityawi -Kahama
JAMES Lembeli ni miongoni mwa wanachama 129 wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
kuwania ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini, ambapo amesema licha ya idadi kubwa ya
vijana kujitokeza haogi na yuko tayari kupambana nao.
Lembeli amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama kwa tiketi
CCM (2005 hadi 2015) kisha kuhamia upinzani na kurejea tena chama tawala,
ambapo Julai 16, 2020 alijitokeza kuchukua fomu kati ya makada 69 waliochukua
fomu hiyo, huku akijimwambafai kupambana na wagombea vijana.
Lembeli aliyechukua fomu hiyo majira ya saa tano za asubuhi
katika ofisi ya CCM Wilaya ya Kahama anajaribu kwa awamu nyingine kuwania
Ubunge Jimbo la Kahama Mjini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, mara baada ya kuchukua
fomu hiyo, Lembeli alisema kuwa ameamua kugombea Ubunge katika jimbo hilo kwa
tiketi ya CCM kwa kuwa vigezo anavyo huku akijinasibu yupo tayari kupamba na vijana katika uchaguzi
huo.
“Timu ikicheza
uwanjani lazima wachezaji wote wawe wazuri na katika mchezo hakuna mzee pia na
mimi nipo tayari kwa mapambano ingawa wengi wa wapinzani wangu waliochukua fomu
hizo kupituia chama cha Mapunduzi ni vijana,” amesema.
Aidha amesema pindi ikitokea baadhi ya watu kutaka kufahamu
alichosahau Bungeni, amedai hakuna alichosahau zaidi ya utashi alionao wa
kuhitaji kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kahama pindi akipata ridhaa ya kuwatumikia kwa
awamu nyingine.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emmanuel
Mbamange, alisema hadi kufikia jana kuna wana CCM 69 waliochukua fomu katika
Jimbo la Kahama Mjini ambapo kati yao Nane ni wanawake.
Mbamange alisema Jimbo la Msalala lina watia nia 43 ambapo
kati yao mwanamke ni mmoja,huku Jimbo la Ushetu wakijitokeza 17 miongoni mwao
wanawake ni wawili.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464