Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.
Amendika historia kwa kuwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha ''Wings of Gold'' au ''mbawa za dhahabu'', baadae mwezi huu wa Julai, kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa Alhamisi wiki hii na Mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi za majini.
Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi "BZ," au "Bravo Zulu,"neno linalotumiwa na wanajeshi -wanamaji , linalomaanisha "umefanya vyema."
"BZ kwa Lt. j.g. Madeline Swegle kwa kumaliza mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi (ya mashambulio) ya anga,"aliandika Mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini. "Swegle ni @Mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anayetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea Mbawa za dhabahabu baadae mwezi huu .
HOOYAH!", uliandikwa ujumbe wa mkuu huyupo wa mafunzo.
Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kumsusu rubani huyu mpya, Swegle kwa sasa yuko katika kituo cha mafunzi cha Redhawks Squadron (VT) 21 katika kituo cha Ndege za vita vya majini -Naval Air Station cha Kingsville kilichopo Texas.
Picha ambazo ziliambatana na twitter ya kikosi cha majini ya kusherehekea mafanikio ya kihistoria ya Bi Swegle zilichukuliwa baada ya safari yake ya mwisho ya ndege ya Mkakati wa mashambulizi ya kivita.
Haifahamiki wazi ni wapi Swegle atakwenda baada ya mafanikio hayo, lakini kama mhitimu wa mpango wa mafunzo ataweza kuendesha ndege za mmapigano ya kimkakati ya ndege azinazotumiwa na wanamaji za kijeshi, kama vile the F/A-18E/F Super Hornet na F-35C Lighting II Joint Strike Fighter.
Swegle, ambaye alihitimu katika Shule ya mafunzo ya jeshi la majini nchini Marekani -US Naval Academy , 2017, anafuata nyayo za wanawake wengine mashuhuri wanajeshi kama vile Kapteni Rosemary Mariner, mmoja wa waanzilishi wa jeshi la anga ambaye alikuwa mmoja wa wanawake marubani walioendesha ndege ya mkakati wa kijeshi mwaka 1974.
Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani
Wengine waliomtangulia na kufanya vyema ni pamoja na Sajenti Martha McSally, Luteni Kanali mstaafu wa Air Force ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza katika jeshi la Marekani kuendesha ndege ya kijeshi katika vita, na Luteni Komandoo Brenda Robinson, ambaye alikuwa rubani wa kwanza mwanamke mweusi kuendesha ndege ya majini, mwaka 1980.
Mafanikio ya kihistoria ya Swegle yanakuja wakati kikosi cha majini cha Marekani kikichukua hatua ngumu ya kushughuliakia ubaguzi wa rangi ndani ya kikosi hicho, huku kukiwa na hofu nchini kote nchini Marekani juu ya ukosefu wa haki dhidi ya watu weusi na pia katika utoaji wa ajira.
Mwezi uliopita wakuu wa kikosi cha wanamaji nchini humo alisema: "kilibaini na kuondoa vikwazo vya rangi na kuboresha ujumuishwaji wa watu wa rangi tofauti katika kikosi cha majini ."