Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo
ZOEZI la upigaji na kuhesabu kura za maoni kwa watia nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi za ubunge linaendelea katika majimbo mbalimbali nchini ili kupata wateuliwa watakaokipeperusha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Haya ni baadhi ya matokeo ya kura hizo yaliyothibitishwa na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini hadi muda huu.
Zoezi la kuhesabu kura katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa
limekamilika na Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ameibuka mshindi kwa kupata
kura 453.
Watia nia wengine na kura zao kwenye mabano ni Kiyoyo (16), Mwilinge (5), Kidunye (5),
Kalinga (4), Mfilinge (4), Kushoka (0), Chengula (0), Gange (0).
Zoezi la kuhesabu kura za maoni, Jimbo la Kisarawe
limekamilika na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameibuka mshindi.
Selemani Jafo (588), Hassan Bangusilo (1), Fransis Gosbert (1), Mohamed
Masenga (1), Ally Goha (2), Zemba Mumbi (2), Zainabu Zowange (2), Chaulembo (3)
Abbas Tarimba
Katika kura za maoni Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba
ameongoza kwa kupata kura
171, akifuatiwa na Idd Azann kura 77, George Wanyama 32 huku mbunge anayemaliza
muda wake Maulid Mtulia akipata kura 11.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Katika Jimbo la Nzega Mjini, Bashe amewashinda watia nia
wenzake 12 kwa kupata kura 367 kati ya kura 376
zilizopigwa, sawa na asilimia 97.
Hawa Ghasia (Kulia)
Hawa ameongoza kura za maoni jimbo la Mtwara Vijijini
kwa kupata kura 440, huku anaemfuatia akipata kura 191 Seleman Mwamba.
Jimbo hilo lilikuwa linawaniwa na watia nia 14, huku jumla ya kura halali zilizopigwa na wajumbe ni 847.
Jimbo hilo lilikuwa linawaniwa na watia nia 14, huku jumla ya kura halali zilizopigwa na wajumbe ni 847.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Awesso
Aliyekuwa mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amefanikiwa
kushinda mchakato wa kura za maoni kwa kupata kura 135.