Jeshi la polisi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, linamshikilia mtu mmoja mjumbe wa chama cha ushirika cha Mlingoti wilayani humo, Bwana Hamidu Mohamed kwa tuhuma za kuiba dawa za kupulizia mikorosho ya wakulima aina ya Sulphur ambayo ilitolewa kwa ajili ya kukopesha wakulima kupitia chama hicho.
Katika kikao na viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Tunduru, mkuu wa wilaya hiyo, Bwana Julius Mtatiro pamoja na kuamuru mtuhumiwa huyo kulipa mifuko yote aliyouza kabla ya kufikishwa mahakamani lakini pia amesema vyombo vya dola vitaendelea kuwasaka wahusika wengine.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464