Mtia nia ya ubunge Jimbo la Musoma Vijijini kwa tiketi ya CCM, Steven Tumaini Machumu.
Na Mwandishi Wetu–Shinyanga Press Club Blog
NI Dhahiri! majina makubwa na mashuhuri yakiwemo ya wasomi wakubwa nchini yanayotajwa kuutaka ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara, hayawatishi wala kuwazuia raia wengine wa kawaida wenye nia ya dhati ya kuliwakilisha jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hii ni baada ya Mwanaharakati wa Maendeleo
jimboni humo, Steven Machumu kuingiza miguu yake kwenye vita ya kusaka nafasi ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.
Machumu ambaye ni
mwanaharakati wa maendeleo na mikakati mbalimbali ya kupunguza umaskini jimboni
humo kwa miaka nane sasa, ametangaza nia ya kugombea ubunge huo kupimana ubavu na Profesa Sospeter Mhongo anayetetea nafasi hiyo pamoja na
majina mengine makubwa ya wasomi wakiwemo maprofesa wanaotajwa kwa sasa.
Machumu
Machumu ambaye ni Mwenyekiti wa Nyanja Economic Investment Trust Fund (NEIT) inayotekeleza
miradi yake katika wilaya za Musoma na Rorya, ametangaza nia yake hiyo Julai 9, 2020 mjini Shinyanga wakati akizungumza na Shinyanga Press Club Blog, na kueleza kuwa ndiye mwenye nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi
wa jimbo hilo waliogubikwa na umaskini kwani amekuwa akifanya hivyo kwa muda
mrefu sasa kuliko wanasiasa wengine ambao wanakwenda kutafuta ajira za kisiasa.
Amesema kwa sasa ni kama jimbo hilo limepoteza dira na hakuna mwanasiasa
mwenye mkakati wa dhati kulikomboa na umaskini, tofauti na yeye ambaye mwaka
2013 alikuja na mkakati kupitia andiko lililopitishwa na baraza la madiwani wa
halmashauri ya Musoma Vijijini kama mradi wa maendeleo, ambapo baadae
walifanikiwa kuanzisha vikundi vya kusaidia kupunguza umaskini.
Ameenda mbali na kubainisha
kuwa endapo atafanikiwa kuipeperusha bendera ya CCM basi kipaumbele chake jimb
oni humo kitakuwa ni elimu, uwekezaji na akiba na kujenga dira ya jimbo kwani
ndivyo msingi wa maendeleo ya jamii ikizingatiwa kwamba jimbo hilo halina
uwekezaji binafsi.
“Nina wiwa kwa mapana na
ujasiri mkubwa kutokana na harakati mbalimbali za kimaendeleo katika jimbo letu
nilizozitekeleza, nina utofauti na wanasiasa wengi wanaouhitaji ubunge kwa
sababu nikiona msururu wa hao watia nia wengi wanataka ajira za kisiasa lakini
hakuna Mwana Musoma Vijijini asiyetambua juhudi zangu za kuwaletea maendeleo.
“Ninajivunia rekodi kubwa ya
mambo ambayo nimeyafanya tofauti na wenzangu wanaokwenda bila chochote, katika
harakati hizi nimethibitisha kwa dhati kwa vitendo na ushahidi mkubwa katika
jamii yangu. Ni mtu wa kwanza niliyetoa semina elekezi ya kuwasaidia
wakulima zaidi ya 300 kwenye jimbo hilo ili kufanya kilimo bora chenye tija na
uzalishaji mkubwa na tulifanikisha kupata mifuko 600 ya mbole kutoka Minjingu,”
alisema.
Machumu
anajivunia juhudi zake zilizowezesha kupeleka wafadhili kuomba shamba la Bugwema, kufanya
tathmini ya wajane, yatima, wazee wasiojiweza na watu wenye ulemavu ambapo
takribani watu 5,000 wako kwenye mpango wa kusaidiwa.
Pia ameisaidia jamii ya
Musoma vijijini kwa kilimo biashara kupitia program ya elimu ya fedha na
ujasiriamali, kuanzisha program ya kusaidia elimu ya msingi na dhana za kilimo
kwa kushirikiana na wadau, ambapo ameandika vitabu saba ikiwemo kuboresha
elimu, kutambua changamoto za kimaendeleo jimboni humo na kwamba hakufanya kwa
nia ya kutafuta umaarufu bali nia ya dhati ya kuwainua wananchi.
“Nimekuwa karibu nao kwa
sababu hakuna mwanasiasa mwenye nia ya dhati ya kulikomboa jimbo letu na janga
la umaskini, lakini mimi baada ya jitihada zote hizo nilibaini kwamba watu
hawana mitaji nikatembelea baadhi ya benki nikaja na mpango mkakati wa kufungua
huduma ya kibenki kila kata jimboni humo (Rural Financial Bank Outlet) ambao
umeanza utekelezaji,” alisema.
Machumu alipofika bungeni kuwasilisha mikakati yake ya kuwasaidia wananchi
Sehemu ya kikundi cha kupunguza umaskini jimboni humo kilichoanzishwa na Machumu
Baadhi ya watoto yatima, wajane na watu wenye ulemavu kutoka jimboni humo walio kwenye mpango wa kusaidiwa kupitia juhudi za Machumu wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la pamoja Jijini Dodoma
Machumu akiwa katika majukumu yake
Sehemu ya vikundi vilivyoko kwenye mpango mkakati wa kuanzisha huduma za kibenki katika kila kata jimboni humo vilivyoanzishwa na mwanaharakati huyo