MWANDISHI WA HABARI ASHEREHEKEA ''BIRTHDAY' YAKE NA AKINAMAMA WAJAWAZITO HOSPITALINI KOLANDOTO

Mtangazaji wa Radio Faraja FM, Josephine Charles akimlisha kipande cha keki mmojawapo wa akina mama wajawazito katika hospitali ya Kolandoto leo Julai 23, 2020.

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Matangazo Radio Faraja FM ya mjini Shinyanga, Josephine Charles, amesheherekea siku yake ya kuzaliwa katika hospitali ya Kolandoto.

Leo Julai 23, 2020 Mwandishi huyo Josephine Charles ametimiza miaka yake kadhaa ya kuzaliwa, ambapo ameamua kusheherekea na wajawazito, pamoja na akina mama ambao wamejifungua watoto wao siku ya leo kwenye hospitali hiyo ya Kolandoto.

Amesema tangu mwaka jana amekuwa na kawaida ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hospitalini, ambapo mwaka huo alisheherekea na akina mama waliojifungua watoto katika hospitali ya rufani mkoani Shinyanga, pamoja na kutoa zawadi mbalimbali.

"Leo nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa na wajawazito pamoja na akina mama ambao wamejifungua watoto wao katika hospitali hii ya Kolandoto, pamoja na kula nao keki na kuwapatia sabuni za kufulia, kuogea pamoja na mafuta ya watoto wachanga," amesema Josephine.

"Pia natoa wito kwa wajawazito mkoani Shinyanga wajenge utamaduni wa kujifungulia watoto hospitalini maeneo ambayo ni salama, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi," ameongeza.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto, Zephania Msunza, amempongeza mwana habari huyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na wajawazito na akina mama waliojifungua watoto, na kubainisha kitendo hicho kinapaswa kuigwa, na siyo kwenda kufanya anasa ikiwamo kunywa pombe.

Amesema watu wengi wange kuwa wakisheherekea siku yao ya kuzaliwa hospitalini, changamoto nyingi za uhaba wa vifaa ingepungua, na kutoa wito kwa wengine kufanya hivyo ili kuboresha huduma za kiafya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Muonekano wa keki. 
Josephine Charles akikata keki.
Josephine Charles akikwalisha keki wajawazito katika hospitali ya Kolandoto kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea, kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Zephania Msunza.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea, kwa muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Christina Richard.
Josephine Charles, kushoto akiwalisha Keki wafanyakazi wenzake wa Radio Faraja.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji keki likiendelea.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Zephania Masunza, kulia, akimlisha Keki Josephine Charles.
Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
Awali mwandishi wa habari kutoka kituo cha Matangazo Radio Faraja mjini Shinyanga Josephine Charles, wapili kutoka kushoto akiwalisi na baadhi ya wafanyakazi wenzake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa katika hospitali ya Kolandoto.
Josepheni Charles wa kwanza kushoto akiimbiwa nyimbo ya Happy birthday.
Josephine Charles watatu kutoka kushoto, akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake pamoja na mganga mfawidhi na Muuguzi Mfawidhi katika hospitali ya Kolandoto mara baada ya kumaliza kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hospitalini hapo.

Picha na Marco Maduhu





































































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464