DAKTARI AFIKISHWA MAHAKAMANI TUHUMA ZA KUBAKA NA KUMPA UJAUZITO MWANAE



Na Joctan Myefu
Mwanafunzi wa Chuo Cha Udaktari wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Mkazi wa Mburahati Jijini Dar es salaam na Itunduma kata ya Mtwango wilaya na Mkoa wa Njombe amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake na kumsababishia ujauzito.

Akimsomea Mashitaka matano yanayomkabili mshitakiwa huyo Mwendesha Mashitaka wa Serikali Bi.Matrida Manja amesema mshitakiwa Joshua Mhema (26) alitenda makosa hayo katika nyakati tofauti Kati ya tarehe isiyojulikana kubaka na shitaka la pili la kubaka alitenda Mei 06/na Mei 26 na kosa la tatu na la nne la kubaka alitenda Mei 27 ambapo tarehe hiyo 27/05/2020 alitenda kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi huyo wa kidato Cha tatu . 
Mshitakiwa alikana Mashitaka yote matano ambapo Mwanasheria wa Serikali Bi.Manja amesema mashitaka yote yanaangukia katika sura ya 130 (1&2) e kanuni ya adhabu na mwenendo wa makosa namba 16 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2016. 

Bi.Manja ameiambia Mahakama kuwa makosa yote hayo matano yanadhamana. 

Mh.Matrida Kayombo alimuuliza mshitakiwa iwapo anao wadhamini wawili wanaotambulika na kufahamika wenye dhamana ya Mali isiyohamishika yenye thamani ya sh.Milioni 15. 

Kesho hiyo imeahirishwa hadi agosti 05 mwaka huu 2020 kwa kuanza kusikilizwa kwa kutolea ushahidi na Mtuhumiwa amepelekwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464