Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba (katikati) akiiingia ukumbini wakati wa sherehe ya Polisi Day Family. Kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo, Davis Msangi.
Na Marco Maduhu -Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, ameonya kuwapo na migogoro ya ndoa kwa familia za askari, kitendo ambacho amedai hapendezwi nacho na hataki kusikia kuendelea kwa migogoro hiyo, na kuwataka amani itawale katika miji yao ndipo wataweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amebainisha hayo jana Julai 31, 2020 kwenye sherehe ya Polisi Family day, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyakahara mjini Shinyanga, iliyohusisha familia za askari Polisi kutoka wilaya zote mkoa huo.
Amesema ili askari afanye kazi zake kwa ufanisi za kulinda usalama wa raia na mali zake, lazima ndoa yake kwanza iwe na amani, na kuwataka askari hao wapendane na wake zao na kuondoa tofauti walizo kuwa nazo hapo awali, ili familia zao zitawaliwe na furaha.
“Katika mkoa wangu wa Shinyanga sitaki kusikia askari wangu wana migogoro ya ndoa katika familia zao, hivi karibuni tu kulitokea tukio la Askari kukatwa sehemu za siri na mkewake, sitaki kabisa vitendo vya namna hii vijirudie, bali pendaneni na wake zenu ndipo mtaweza kufanya kazi zenu kwa ufanisi,” amesema Magiligimba.
“Na nyie wake za askari mnatakiwa muwapende waume zenu pamoja na kazi zao wanazozifanya, siyo mumewako anatoka kazini usiku una anza kumrushia maneno badala ya kumpa pole na kazi, pia nitatembelea wilaya zote kufanya vikao na wake za askari ili kuzungumza nao na kuziweka sawa ndoa zao,” ameongeza.
Aidha amesema kama familia yoyote ya Askari ambayo ina migogoro wafike kwenye ofisi yake wazungumze ili kutatua mgogoro huo, na siyo kukaa kimya na hatimaye kujichukulia sheria mkononi na kutokea mapigano au askari kujipiga risasi.
Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga (RCO), Davis Msangi, amewataka askari wa kuelekea kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu, wazingatie maadili ya kazi zao pamoja na sheria za uchaguzi, kwa kuhakikisha uchaguzi una malizika kwa amani kuanzia kipindi cha Kampeni hadi matokeo kutangazwa.
Amesema askari ni sehemu wa wasimamizi wa uchaguzi, hivyo wanapaswa kusimamia mikusanyiko mbalimbali ya kisiasa kipindi cha kampeni, pamoja na kulinda viongozi wote wa kisiasa na wanachama wao bila ya kujali itikadi zao za siasa, ambapo kazi yao kubwa ni kuhakikisha amani inatawala kwenye uchaguzi mkuu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Debora Magiligimba akizungumza kwenye hafla ya Polisi Family Day na kuonya migogoro ya ndoa kwa familia za askari.
Mkuu wa upelelezi mkoani Shinyanga Davis Msangi, akitoa elimu ya uchaguzi mkuu kwa Askari.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Maaskari wakiwa kwenye Sherehe ya Polisi family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Familia za Askari zikiwa kwenye sherehe ya Polisi Family Day.
Mahaba ndani ya Polisi Family Day,
Ndafu ikikatwa kwa ajili ya Familia za Askari kusheherekea siku ya Polisi Family Day.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba, kushoto akionyesha picha aliyochorwa ambayo amepewa Zawadi na Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hiyo, kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Grace Salia.
Wana-kamati wakimpatia Zawadi ya Vitenge Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba.
Super Kwata Bendi wakitoa burudani kwenye sherehe hiyo ya Polisi Family Day.
Super Kwata Bendi wakitoa burudani kwa Stly ya kucheza Kikangi Lugola, inaitwa "cheza Kikangi- Kangi"
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba, akitoa burudani kwenye sherehe hiyo ya Polisi Family Day.
Awali Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (katikati) Debora Magiligimba akiingia ukumbini kwenye sherehe ya Polisi Family Day..
Picha zote na Marco Maduhu- Shinyanga