RAIS MAGUFULI AZITAKA TAASISI ZINAZODAIWA NA SUMA JKT KUILIPA SH BILIONI 11 NDANI YA SIKU 14





RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli leo Julai 22, 2020 ametoa siku 14 (wiki mbili) kwa taasisi zote za Serikali na Binafsi zinazodaiwa na SUMA JKT kuilipa mara moja, huku akitahadharisha kwa taasisi yoyote itakayoshindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Julai 22, 2020 wakati akifungua jengo la ghorofa nane la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ambapo amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa zoezi hilo.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, SUMA JKT inazidai taasisi mbalimbali ilizofanya nazo kazi  Jumla ya Sh Bilioni 11.

"Ndani ya wiki mbili, taasisi zote zinazodaiwa  iwe wizara ya fedha, iwe ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, taasisi za serikali ama binafsi hizo Bilioni 11 zilipwe. 

"Waziri Mkuu fuatilia watakaoacha kulipa ndani ya wiki mbili nijulishe mahali popote nitakapokuwa nafanya kampeni, nijue taasisi gani imekataa kulipa," amesema.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464