Hayo ameyazungumza mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea kiwanda hicho katika hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora.
Amesema kuwa kiwanda hicho kinatoa mchango mkubwa kwa kuchangia kodi serikalini bilioni 30.Amesema kuwa serikali imetoa bilioni 26 kwa ajili ya mradi mkubwa wa umeme katika eneo la Dege ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu ili kuongeza uzalishaji katika kiwanda hicho.
DC Msafiri amesema pia kukamilika mradi mkubwa wa umeme sambamba na mchakato wa kufunga mfumo wa gesi wilayani humo kutachochea uwekezaji na uzalishaji katika viwanda na kuongeza pato la taifa.
Amesema kuwa serikali imetoa bilioni 26 kwa ajili ya mradi mkubwa wa umeme katika eneo la Dege ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu ili kuongeza uzalishaji katika kiwanda hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akipanda mti wa kumbukumbu katika kiwanda cha Lake Cement. Wafanyakazi wa Kiwanda cha Lake Cement wakiwa wamejipanga tayari kwa kumpokea Mkuu wa Wilaya Kigamboni Sarah Msafiri.
“Nataka kuwahakikishie kuwa mradi wa umeme utakapo kamilika mwishoni mwa mwezi ujayo (Agosti) tutawaletea Megawati 5 ili kuongeza uzalishaji zaidi na najua mnajua tumeanza mchakato wa kuleta gesi katika maeneo haya ya viwanda kwani serikali imepima ‘block’ 400 za viwanda hivyo kiwanda cha Lake Cement kitakuwa wanufaika wakwanza” amesema Msafiri
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri katikati akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Mkuu wa Uzalishaji wa kiwanda cha Lake Cement, Biswajeet Mallik kulia pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Amesema kiwanda hicho kimekuwa kikilipa kodi Bilioni 30 kwa mwaka hivyo ni kiwanda ambacho kinachochea ukuaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa saruji inayozalishwa katika kiwanda hicho imekuwa ikitumika katika miradi mikubwa ya serikali kama mradi wa uzalishaji wa umeme Rufiji, ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa madaraja makubwa na ujezi wa barabara za juu Ubungo.
Katika Hafla hiyo msanii wa Bongo Fleva, Barnaba alitoa burudani kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na wageni waalikwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri.
DC Msafiri ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea na uzalishaji na hawakupunguza wafanyakazi katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Lake Cement, Julieth Domel.
Mkuu wa Uzalishaji wa Kiwanda cha Lake Cement, Biswajeet Mallik.
Hata hivyo DC Msafiri amewataka vijana ambao wameajiriwa katika kiwanda hicho kutoshiriki katika kuvuruga amani ya nchi katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa upande wa Mkuu wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Biswajeet Mallik, amesema kuwa katika kipindi cha janga la corona walijitahidi kutoa elimu kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na hakuna mtu aliyepata maambukizo ya ugonjwa huo na kwa sasa wamejipanga kuongeza uzalishaji.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464