SHEIKH BALILUSA AONGOZA SWALA YA EID AL-ADHA, ATAKA AMANI ITAWALE UCHAGUZI MKUU

 
Waumini wa Dini ya Kiislam mjini Shinyanga wakiendelea na swalaa ya Eid Al-Adha leo Julai 31, 2020 katika uwanja wa Sabasaba mjini humo.


Na Marco Maduhu - Shinyanga

Shekh Balilusa Khamisi wa mjini Shinyanga, amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa hapa nchini pamoja na wanachama wao, kudumisha amani katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba mwaka huu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais.

Amebainisha hayo leo mara baada ya kumaliza kuongoza swalaa kwenye sikukuu ya kuchinja (Eid Al Adha) iliyofanyika kwenye uwanja wa uhuru (Sabasaba) mjini Shinyanga, kuwa matarajio ya viongozi wa dini ni kuona uchaguzi mkuu unakuwa tulivu na amani, na kusiwapo vurugu zozote zile za uvunjifu wa amani.

Sheikh Khamisi ambaye pia ni mwenyekiti wa amani mkoa wa Shinyanga, amesema viongozi wa siasa pamoja na wanachama wao, wanapaswa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na siyo maslahi yao binafsi katika kipindi cha uchaguzi mkuu, na kutofanya vurugu ambazo zitavunja amani ya nchi na kuingia kwenye machafuko.

“Sisi kama viongozi wa dini tunawaomba sana viongozi wa kisiasa hapa nchi pamoja na wanachama wao, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, watangulize maslahi ya taifa na siyo maslahi yao binafsi, ili kulinda amani ya nchi yetu na kutofanya vurugu zozote kwenye uchaguzi,” amesema Shekh Khamisi.

Katika hatua nyingine amewataka wakuu wote wa shule binafsi kutowanyima wanafunzi muda wa kwenda kuswali masomo ya dini, kwa madai ya kufidishia muda uliopotea wakati wa kipindi cha likizo ya Corona, bali wawa ruhusu ili wapate masomo hayo ya kiimani ambayo yatawajenga kimaadili.

Naye Mjumbe wa Baraza la Mashekh mjini Shinyanga, Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaidha amewataka waumini wa dini hiyo ya kiislam hasa vijana, kuzingatia miiko na sheria ya dini hiyo ili kutoporomoka kimaadili, pamoja na kuacha kuzaa watoto kabla ya kufunga ndoa na kutolelewa na majimama.

Aidha amesema baadhi ya vijana wa dini hiyo hawana maadili kabisa, ambapo wamekuwa wakifanya uzizi na kuzaa watoto nje ya ndoa, kutovaa mavazi ya heshima, kunyoa mitindo ya nywele, pamoja na kupenda mtelemko na kwenda kuoa wanawake wenye pesa bila hata ya kujali tabia zao wala umri bali wao wanajali pesa tu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Shekh Balilusa Khamis akizungumza mara baada ya kumaliza kuongoza swalaa ya Eid Al- Adha katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga.

Shekh Balilusa Khamisi akiongoza maombi kwenye swala ya Eid Al Adha kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga.

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye maombi ya Ibada ya Eid Al Adha katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga.

Waumini wa dini ya Kiislam mjini Shinyanga wakiendelea na Swala ya Iddi uwanja wa Sabasaba.

Mjumbe wa baraza la Mashekh mjini Shinyanga, Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaidha kwenye swala ya Eid Al- Adha.


Swala ya Eid ikiendelea.

Swala ya Eid ikiendelea

Waumini wa dini ya Kiislam wakiendelea na swala ya Eid

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye maombi ya Eid Al -Adha.

Maombi yakiendelea.


Picha na Marco Maduhu














Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464