Mratibu wa Kituo cha kufundishia Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Grace Maleko akisoma taarifa ya kituo hicho kwenye kikao cha wajumbe wa Baraza la chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
Naibu makamu mkuu wa chuo utawala na fedha Prof. Fredy Kilima amesema watahakikisha kituo hicho kinaendeleo kuboreshwa ili kuondoa utofauti kati ya chuo cha Ushirika Moshi na kituo cha Kizumbi.
Na Shinyanga Press Club Blog
Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi limetembelea eneo linalomilikiwa na Kituo cha ufundishaji Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kujionea uharibifu wa mazingira na uvamizi wa maeneo ya kituo hicho unaofanywa na wanakijiji.
Uvamizi wa maeneo ya kituo hicho umekuwa ukisababisha migogoro kati ya kituo hicho na wanakijiji ambao wanakata miti na kuchoma moto msitu kwa lengo la kutafuta kuni pamoja na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya eneo la chuo.
Mwenyekiti wa baraza hilo George Yambesi amekipongeza kituo hicho kwa kuwa na mazingira mazuri yenye miti ya asili na amewataka kuendelea kuitunza miti ya asili ili iendelee kuwa kivutio kikubwa kwenye chuo hicho na kusisitiza kuwa uvamizi unaofanyika usije kuwa chanzo cha kumaliza miti hiyo.
Amesema wanaendelea na maboresho ya kituo hicho ikiwemo kuboresha miundombinu na kuongeza watumishi,huku akiwataka watumishi wa kituo hicho kutojiona wameachwa peke yao bali ni kutokana na changamoto za fedha.
Mratibu wa Kituo cha kufundishia Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Grace Maleko ambacho kiko chini ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, amesema wanakabiliwa na changamoto ya uvamizi wa maeneo, uchomaji msitu na ukataji miti ambao unatishia usalama wao.
Akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa baraza la chuo kikuu Moshi kilichofanyika kwenye kituo cha Kizumbi Shinyanga amesema wanakijiji wamekuwa wakivamia maeneo na kufanya shughuli za kibinadamu .
Maleko amesema changamoto hizo zinatokana na eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 107 kutokuwa na uzio hivyo wanakijiji wanatumia fursa hiyo kufanya uvamizi na kusababisha migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama kutokana na kuchoma moto.
Makamu mkuu wa chuo cha Ushirika Moshi Prof.Alfred Sife amesema mpango uliopo ni kuwa na matumizi bora ya ardhi kwani eneo hilo lina hati miliki na kwamba wanalimiliki kihalali tangu mwaka 1968 na kwamba kwa kushirikiana na serikali watamaliza uvamizi huo.
Wajumbe wa baraza wakiendelea na kikao
Jengo la utawala la kituo cha kujifunzia Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo -taaluma Dkt.Goodluck Mmary akieleza mafanikio yaliyofikiwa katika kituo cha kufundishia Kizumbi.
Wajumbe wa baraza wakitembelea maeneo ya kituo hicho
Jengo la Zahanati katika kituo cha kufundishia Kizumbi
Wajumbe wa baraza na watumishi wa kituo cha kufundishia Kizumbi wakiangalia maeneo ya mpaka wa kituo hicho.
Zoezi la kutembelea maeneo linaendelea
Kikao cha wajumbe wa baraza kikiendelea
Zoezi linaendelea
Wajumbe wa baraza ,watumishi na viongozi wa serikali ya wanafunzi kituo cha kufundishia Kizumbi
Watumishi wa afya wakiwa kazini katika zahanati ya kituo cha Kizumbi
Zoezi linaendelea
Picha ya pamoja
Makamu mkuu wa chuo cha Ushirika Moshi Prof.Alfred Sife aliyesimama mkono wa kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la chuo George Yambesi
Watumishi wa kituo hicho
Wajumbe wakiangalia maeneo ya kituo hicho
Viongozi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi wakifuatilia taarifa iliyotolewa.
Wajumbe wakifuatilia
Wajumbe wanaendelea namazungumzo
Makamu mkuu wa chuo cha Ushirika Moshi Prof.Alfred Sife akiwasalimia wajumbe
Charles Samson afisa utumishi kituo cha kufundishia Kizumbi akitoa neno la shukrani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464