Mtia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga aliyesimama mkono wa kulia Emmanuel Ntobi akimkabidhi fomu Katibu wa Jimbo la Shinyanga Joseph Ndatala ikiwa ni siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo.
Na Mwandishi wetu Shinyanga Press Club Blog
Joto la uchaguzi mkuu limezidi kushika kasi katika mikoa mbalimbali hapa nchini,ambapo baadhi ya watia nia ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Shinyanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamerudisha fomu za kuwania kuteuliwa kugombea nafasi hiyo huku kila mmoja akijigamba kuwa ataleta mabadiliko makubwa.
Zoezi la kurudisha fomu hizo limefanyika leo Julai 10 katika ofisi za Chadema mkoa wa Shinyanga ikiwa ni siku ya mwisho kwa chama hicho wagombea waliotia nia kugombea ubunge kurudisha fomu,huku Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga akiwa ni wa kwanza kurudisha fomu hiyo .
Akizungumza wakati wa kupokea fomu za watia nia wa kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Shinyanga Katibu wa jimbo la Shinyanga wa Chama cha Chadema Joseph Ndatala,amesema kuwa waliotia nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga ni 11 lakini waliochukuwa fomu ni tisa.
Katibu Ndatala aliwataja waliochukuwa fomu ni Emmanuel Ntobi,Salome Makamba,Nichoraus Luhende,Samson Nghwagi,Hassan Salim,Zena Gulam,Zainab Kheri na Mch.Jilala Fumbuka na kubainisha zoezi lilikuwa huru kwa kila Mwanachama .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mtia nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Emmanuel Ntobi ,amesema iwapo atapewa ridhaa na wanachama ya kuwa mgombea wa jimbo hilo atahakikisha anafanya mabadiliko makubwa ya maendeleo.
Ntobi ambaye pia alikuwa diwani wa Kata ya Ngokolo 2015-2020 aliyemaliza muda wake,amesema kilichomsukuma kuamuwa kugombea ubunge ni kutokana na jimbo hilo kuendelea kudidimia na kushindwa kupiga hatua ya maendeleo huku akieleza kuwa iwapo atakuwa mbunge atahakikisha Shinyanga inakuwa na chuo kikuu.
Naye aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chadema Salome Makamba ambaye ameweka nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga,amesema mkoa wa Shinyanga ni mkoa wa nne Kitaifa kuchangia pato la Taifa lakini hakuna maendeleo,amesema iwapo atapewa nafasi hiyo atafanya kazi kubwa ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na elimu.
Mtia nia mwingine wa ubunge jimbo la Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la vijana wilaya ya Shinyanga Samson Nghwagi alisema kiongozi bora ni yule anayerudi kusikiliza kero za wananchi kwa kurudi kwa wananchi na kuwaomba kumpa ridhaa ili afanye kazi.
Mtia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza na wanachama baada ya kurudisha fomu ya kugombea ubunge iwapo atateuliwa na Chama.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wakiwa katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Shinyanga.
Mtia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Salome Makamba ambaye pia alikuwa Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chadema akikabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa na Chama kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi ambaye pia ni mtia nia ya kugombea Ubunge jimbo la Shinyanga akizungumza na wanachama baada ya kurudisha fomu.
Mtia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Samson Nghwagi akikabidhi fomu yake ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga iwapo atapitishwa na Chama chake.
Baadhi ya wanachama wa Chadema wakishangilia wakati Mtia nia ya kugombea Ubunge jimbo la Shinyanga Salome Makamba wakati alipokuwa anarudisha fomu
Viongozi na wanachama wa Chadema wakishuhudia watia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga wakiendelea kurudisha fomu.
Mtia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Salome
Makamba akizungumza na wanachama baada ya kurudisha fomu ya kugombea ubunge iwapo atateuliwa na Chama.
Viongozi na wanachama wa Chadema
Zoezi linaendelea
Msanii wa nyimbo za asili akiwaburudisha viongozi na wanachama wa Chadema wakati zoezi la watia nia kurudisha fomu za kugombea ubunge jimbo la Shinyanga iwapo chama kitamteua mmoja wapo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464