Moja ya madarasa yanayojengwa kupitia juhudi za wadau mbalimbali wakiwemo waimbaji wa nyimbo za injili ili kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu kupata elimu.
Na Mwandishi Wetu - Shinyanga Press Club Blog
WATOTO zaidi ya 300 wanaoishi katika mazingira magumu
wakiwamo yatima na walemavu katika kata ya kagongwa wilayani kahama wameokolewa
katika wimbi la kukosa elimu kwa kujengewa madarasa ya kusomea na wadau wa
elimu wa eneo hilo la kagongwa lengo likiwa ni kuhakikisha watoto hao waliokosa
elimu ya awali wanapata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine nchini.
Majengo hayo ya madarasa yamejengwa kwa ushirikiano wa
waimbaji wa nyimbo za injili na wadau mbalimbali wakiwemo waimbaji wa nyimbo za
injili, Bahati Bukuku na Saulo Maziku ambao wamejitolea mauzo ya albamu zao
zinazouzwa yaende kujenga shule kwa ajili ya watoto wenye mahitaji.
Baadhi ya wanafunzi kutoka kwenye makundi hayo akiwemo
Elizabeth Ernest wameonyesha faraja yao na kuwashukuru wadau, huku mlezi wao Mchungaji
Samwel Bundala aliomba msaada zaidi wa wadau kuendelea kusaidia makundi hayo.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Kahama, Jerome
Lugome ambaye ni Afisa Mtendaji Kata ya Kagongwa wilayani Kahama amesema serikali
imeendelea kujali michango ya wadau katika kuendeleza sekta ya elimu huku
akitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuhakikisha watoto hao wanapata haki
ya elimu na mahitaji mbalimbali.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Saulo Maziku na Bahati Bukuku ambao walihudhuria zoezi hilo
Mchungaji na Mlezi wa watoto hao, Samwel Bundala
Bahati Bukuku
Baadhi ya wananchi waliohudhuria zoezi hilo
Mmoja wa wanafunzi hayo, Elizabeth Ernest
Zoezi la uuzaji Albamu kutoka kwa waimbaji wa injili likiendelea
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama
Mwimbaji wa nyimbo za Injli, Bahati Bukuku
Zoezi likiendelea
Waimbaji wa nyimbo za injili akiwemo Bahati Bukuku (kulia) akishiriki kuuza albamu ambazo mapato yake yatasaidia watoto walio katika mazingira magumu
Wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika zoezi hilo.