YANGA YAMFUTA KAZI KOCHA WAKE, YAMTAKA KUONDOKA NCHINI HARAKA


Kocha Luc Eymael

Na Damian Masyenene
Moja ya mambo yaliyojiri na kuteka hisia za mashabiki wengi wa soka na Watanzania kwa ujumla katika siku ya mwisho ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) iliyohitimishwa jana Julai 26, 2020, ni kitendo cha Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mbelgiji Luc Eymael kuwakashfu wanachama na mashabiki wa Yanga akidaiwa kuwaita mbumbumbu, nyani na wasiojielewa huku pia akisema kuwa mkewe amechoka kuishi Tanzania na yeye hafurahishwi na mazingira yahapa nchini.

Kauli hizo za mbelgiji huyo ambaye amekuwa na vihoja kadha wa kadha katika baadhi ya michezo ya timu hiyo ikiwemo kueleza kuwa anafanyiwa vitendo vya ubaguzi na waamuzi wa Tanzania, hii leo vimemgharimu baada ya kujikuta akifungashiwa virago na waajiri wake.

ambapo leo Julai 27, 2020 Klabu ya Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wakili Simon Patrick imetangaza kuachana na kocha huyo kwa kile kinachoeleza kuumizwa na kauli zake, ambapo imemtaka kuondoka nchini haraka iwezekanavyo.

Soma zaidi maudhui ya barua iliyotolewa leo na Yanga ikieleza kumfuata kazi Kocha wake Mkuu, Luc Eymael.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464