JAMBO YAWAPIGA TAFU VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA WANARIADHA SHINYANGA

Afisa Mauzo wa Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus akimkabidhi jezi Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 jijini Dar es salaam

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji Vinywaji Baridi Jambo Food Products Ltd imetoa msaada wa vifaa vya michezo na fedha kwa wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.

Akizungumza leo Alhamis Agosti 27,2020 Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary amesema Kampuni yao imetoa msaada wa vifaa vya michezo ili kuwapa ari na moyo wanariadha watatu kutoka mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa mwaka 2020.

“Jambo Food Products Ltd ni wadau wakubwa wa michezo,leo tunakabidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi na truck suit na fedha taslimu shilingi 470,000/= kwa ajili ya wanamichezo kutoka mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha kitaifa ili kuwaongezea ari na moyo wa kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo”,amesema Halima.

“Tunaamini kabisa wanamichezo wa mashindano ya riadha watauwakilisha vyema mkoa wa Shinyanga katika kuhakikisha tunapata medali kwenye mashindano ya riadha kitaifa na hata ngazi ya kimataifa”,ameongeza Halima.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe ameishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa mchango wao kwa wanamichezo watatu mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki mashindano ya riadha kitaifa.

Amewataja wanamichezo watakaowakilisha mkoa wa Shinyanga katika Mashindano ya riadha kitaifa kuwa ni Happiness Emmanuel,Magere Joseph na Edward Mashenene ambao wamepatikana kupitia mchujo uliofanyika katika halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga.

Naye Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi ambaye ni Mwalimu wa riadha amesema washiriki wa mashindano ya riadha kitaifa kutoka mkoa wa Shinyanga wameandaliwa vizuri ili kuhakikisha kuwa mkoa wa Shinyanga unajipatia medali kwenye mashindano hayo.

“Licha ya kwamba tuna wanamichezo wazuri lakini bado tunaendelea kuwaandaa ili kuhakikisha tunajipatia medali katika mashindano hayo yanayotarajia kufanyika Septemba 12-13 mwaka 2020”,amesema Mgambi.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus akimkabidhi jezi Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary, wa kwanza kulia ni  Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Mauzo wa Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus akimkabidhi jezi Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary, wa kwanza kulia ni  Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi.
Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary akimkabidhi  shilingi 470,000/= Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus , wa kwanza kulia ni Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi.
Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary akimkabidhi  shilingi 470,000/= Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Taifa Michezo ya Riadha yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus , wa kwanza kulia ni Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe na Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi wakionesha jezi kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. Wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe na Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi wakionesha jezi kwa ajili ya wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Taifa Michezo ya Riadha yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa wanariadha mkoa wa Shinyanga ambapo Kampuni hiyo imetoa msaada wa vifaa vya michezo ili kuwapa ari na moyo wanariadha watatu kutoka mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha kitaifa mwaka 2020. Kushoto ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd. Alodia Ladislaus.
Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd. kwa mchango wa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanamichezo watatu mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki mashindano ya riadha kitaifa.
 Katibu wa Riadha mkoa wa Shinyanga Inyasi Mgambi ambaye ni Mwalimu wa riadha akielezea namna walivyojiandaa ili kuhakikisha kuwa mkoa wa Shinyanga unajipatia medali kwenye mashindano ya riadha kitaifa mwaka 2020.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464